- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Jamal Malinzi
DAR
ES SALAAM, JANUARI 20, 2017;
RAIS wa
Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, amempongeza Rais wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kuteuliwa kuwa Mjumbe wa
Kamati ya Maendeleo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Kwa
mujibu wa taarifa ya Fifa ya Januari 18, 2017, iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa
Fifa, Fatma Samoura, Malinzi ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati hiyo
kuanzia mwaka huu 2017 hadi 2017.
Taarifa
hiyo ilifafanua kuwa, Kamati hiyo inaongozwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al
Khalifa, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka la Asia, ina majukumu ya
kusimamia mipango ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani kote.
Nikiwa
Rais wa RT, nachukua nafasi hii kukupongeza Mheshimiwa Malinzi kwa kuaminiwa
kwako Fifa na kuteuliwa katika nafasi hiyo, uteuzi ambao unaongeza heshima ya
taifa letu katika medani ya michezo.
RT
inakuahidi Bw. Malinzi kuwa tutakupa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji
mwema wa majukumu yako, ndani na nje ya kamati hiyo, ili kuendelea kujenga
taswira nje kwa shirikisho lililokuamini na kukupa jukumu hilo.
Naamini
Fifa haijakosea kukupa ujumbe wa kamati hiyo, kwani umekuwa na taswira za
kimaendeleo, kama ulivyothibitisha katika harakati zako za kukuza soka la
Tanzania katika kipindi kifupi cha uwepo wako madarakani.
Nakutakia
kila la kheri katika nafasi mpya, tukiamini kwa pamoja tutashirikiana nawe
katika majukumu yako kama mjumbe wa kamati hiyo muhimu ya Fifa.
Ahsante
Anthony
Mtaka
Rais RT na
Mjumbe
Kamisheni ya Mipango, Ushauri, Mawasiliano na Mikakati Shirikisho la Riadha la
Kimataifa (IAAF)
Januari
20, 2017
Comments
Post a Comment