- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Dar Es Salaam 20 Jan 2017
BENKI ya
NMB imekubali kutoa fedha kwa ajili ya kujenga 'skimu' kubwa ya mfano ya
umwagiliaji katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
"Maji
ni raslimali muhimu sana inayotoa uhakika wa kuvuna pamoja mbali ya pembejeo na
uhifadhi', alisema Seif Ahmed, afisa mkuu upande wa biashara ya kilimo
(Agribusiness).
"Mkuu
wa Mkoa ninakupongeza wewe na timu yako kwa nia ya kuwaletea wananchi wa Simiyu
maendeleo, " alisema na kuongeza, "Ninawahakikishia kuwa tutawapatia
mkopo huo."
Ahmed
aliahidi kufanya kazi pamoja na Mkoa wa Simiyu kuhakikisha mradi unaleta
mabadiliko ndani ya jamii.
Afisa
Mwakilishi wa Serikali katika NMB,
Domina Feruz, alisema kilimo cha umwagiliaji kitatoa uhakika wa mavuno
na kuwapo uhakika wa marejesho ya mkopo na chakula muda wote wa mwaka",
alisema Afisa huyo.
NMB KUUNGANISHA NGUVU
Alisema
kuwa NMB iko tayari kuwaunganisha na mfadhili wa kimataifa ambaye atawapatia
ufadhili mkubwa zaidi wa kifedha alimradi wanunue zana za kilimo kutoka kwenye
kampuni hiyo.
Ahmed
alisema MMB iko tayari kushirikiana na washirika wengine kama PASS, katika
uandaaji wa mpango wa mradi pamoja na Serikali ya Mkoa wa Simiyu ili mradi
uanze mara moja.
"Ukweli
ni kwamba tukiendelea kusubiri mvua ili tuvune, ni vigumu kupiga hatua kubwa ya
maendeleo na mabenki yanatoa fedha zao kwa woga wa kuzipoteza endapo mvua
haitanyesha," alisema.
Ahmed
aliongeza kuwa skimu ya umwagiliaji itawaunganisha wakulima sio tu kuwapa sauti
moja bali pia kusafirisha mazao yao katika masoko ya nje ya nchi (export
markets).
Tanzania,
katika utawapa wa Mwalimu Nyerere, iliwahi kuwa na kampuni ya uuzaji wa mazao
ya kilimo katika masoko ya kimataifa, GAPEX, ambayo ililiwezesha Taifa kupata
fedha nyingi za kigeni.
KUSHIRIKI UCHIMBAJI MITARO
"Mimi
pamoja na Kamati yangu ya Ulinzi na Usalama mtupangie Kata za kwenda kushiriki
uchimbaji wa mitaro ya umwagiliaji, " alisema RC Mtaka.
RC Mtaka
alisema Mh Rais Magufuli atawashangaa endapo wataomba chakula wakati wana maji
tee pale Busega.
Mh Rais
atatushangaa. Tumeikataa hii aibu Simiyu kuomba chakula wakati tuna maji tele
Busega, nitashirikiana na wananchi mimi na Kamati yangu ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa ikiwa sehemu ya mchango wetu," alisema.
ENEO LA MRADI
Mradi wa
kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji maji utafanyika katika Kata sita
za Wilaya ya Busega zenye ukubwa wa hekta 1,500.
Hata
hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Busega, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Kiloleli, Vumi Magoti, ameshauri kuangalia uwezekano wa kupanua mradi kufikia
hekta 6,000.
"Inawezekana
kupata impact kubwa zaidi endapo tutaweza kuongeza eneo la mradi,"alisema.
Alisema
wananchi wa Busega huwa wanachanga fedha kumlipa mtu awaletee mvua bila kuwa na
uhakika, "huu mradi una uhakika wa kuleta maji, watahamasika kushiriki
kuchimba mitaro," alisema Bw Magoti.
SKIMU KUONGEZA UZALISHAJI WA MPUNGA
Katika
hotuba yake ya ufunguaji wa mkutano huo wa kazi, RC Mtaka alisema, pamoja na mazao mengine,
mradi unalenga kuzalisha zao la mpunga.
AWATAKA NMB KUFUNGUA TAWI BUSEGA
Aliwataka
NMB kuharakisha kufungua tawi lao Wilayani Busega kabla mradi haujaanza ili
kukabiliana na ongezeko la uhitaji wa huduma za kibenki wilayani humo hasa
baada ya mradi kuanza.
Katika
ziara yake, Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu mapema jana asubuhi (19 Jan 2017)
alikubaliwa kupata mkopo mkubwa kutoka Benki ya Maendeleo ya TIB.
Mkopo huo
utasaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji
katika kiwanda cha chaki.
Miradi
mwingine ni ujenzi wa Kiwanda cha uzalishaji wa vifaa vya hospitali
vinavyotokana na mazao ya pamba na upimaji wa viwanja vya makazi, biashara na
taasisi katika eneo la Mperani katika Halmashauri ya Bariadi.
RC Mtaka
na ujumbe wake wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu wanaendelea na
ziara iliyodhamiria kuujenga mkoa wao.
Kamati
hiyo leo asubuhi itatembelea SUMA-JKT na wanategemea kufanya makubaliano
kadhaa.
Comments
Post a Comment