- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Hii ndiyo nyumba ya marehemu Martha Mbega
ambayo imesombwa na maji na kusababisha maafa makubwa.
MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo mjini Mpwapwa
imenifanya nipoteze ndugu watatu kufuatia nyumba waliyokuwa wamelala kusombwa
na mafuriko.
Waliofariki ni Martha Mbega (62) ambaye ni mtoto wa kaka
yangu, na wajukuu zake wawili wa kike Shukuru Chinyanya (16) na Bernadeta
Mabula (6).
Nimeambiwa kwamba maiti zote, ikiwemo nyingine ya mwanamke ambaye
hakuweza kufahamika mara moja, zimepatikana na zimehifadhiwa katika Hospitali
ya Wilaya Mpwapwa.
Wajukuu wengine wawili wa marehemu (kwangu mimi ni vitukuu),
Beka Ulanga (11) na Joseph Mabula (8) walinusurika baada ya kufanikiwa
kukimbia, ambapo inaelezwa kwamba, Joseph alikutwa akiwa amekwea mti yapata
kilometa mbili kutoka eneo la tukio huku mwenzake akikimbilia kwenye nyumba ya jirani umbali wa meta 800.
Mume wa marehemu hakuwepo wakati wa tukio hilo, kwani
alilala kwa mke mdogo.
Nimezungumza kwa simu na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa
(OCD) Mohammmed Rama Mhina ambaye amenithibitishia tukio hilo na kusema bado
wanaendelea kupokea taarifa zaidi.
“Kwa sasa tunaweza kusema ni vifo hivi vinne tu pamoja na
nyumba ya Mzee Mabula (mume wa marehemu Martha Mbega) ambayo imesombwa, lakini bado
hatujasikia zaidi ya hayo,” alisema kamanda Mhina.
Comments
Post a Comment