 |
Diwani
wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi akiangalia namna wanavyoandika
wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi ya Mchanganyika Kata ya Pongwe
Jijini Tanga wakati wa ziara yake
|
Diwani wa Kata ya Pongwe
(CCM) Mbaraka Sadi wa kwanza kushoto akisikiliza kero za wanafunzi
hao.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya
Msingi Mchanganyiko ya Pongwe ya wanafuzi wasiosikia na wenye matatizo
ya ngozi (Albino),Waziri Mfaume kulia akimuonyesha diwani wa Kata ya
Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi maeneo yenye mapori yaliyozunguka shule hiyo
ambayo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi hao wakati wa ziara ya diwani
huyo


WATOTO
wenye ulemavu wa ngozi na wasioona wanaosoma shule ya msingi ya
mchanganyiko ya Pongwe iliyopo Jijini Tanga wapo hatarini kuvamiwa na
watu waovu na kuwafanyia vitendo vya kikatili kutokana kukosa uzio na
sehemu kubwa kuzungukwa na pori ambalo ni hatari kwa usalama wao.
Shule hiyo ambayo inapokea watoto wenye matatizo hayo kutokana mikoa
mbalimbali Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana uzio
huku sehemu kubwa ikipakana na pori jambo ambalo linaweza kusababisha
hatari kwa ustawi wao kielimu.
Hayo yalibainishwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Waziri Mfaume
wakati wa ziara ya Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi
aliyoifanya kuangalia changamoto ambazo zinaikabili na kuona namna ya
kuzipatia ufumbuzi.
Waziri alisema licha ya kufanya jitihada kubwa za kuanza ujenzi wa
uzio huo eneo la mbele ya shule hiyo lakini mpaka sasa hakuna msaada
wowote ambao wamekuwa wakiupata ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo
linatishia usalama wa watoto hao.
Alisema awali changamoto hiyo ilikuwa eneo la mbele ya shule hiyo na
kuona namna ya kulipatia ufumbuzi haraka ikiwa ni mkakati wa kuendelea
kuwavutia wadau kuweza kusaidia lakini suala hilo mpaka sasa limeshindwa
kupatiwa tiba.
“Awali tuliona tuanze kujenga ujenzi wa fensi mbele ya shule hii
lengo likiwa kuwavuta wadau wengine ili kutusaidia lakini tukashindwa
kujenga eneo ambalo ni pori kubwa na hivyo ni hatari kwa usalama wa
wanafunzi “Alisema.
Aidha alisema licha ya jambo hilo lakini lingine ambalo limekuwa
kikwazo kwao kwenye suala la usalama ni walinzi ambao wanalinda shule
hiyo ambao ni mgambo wanaotumia virungu na mapango ambazo ni silaha
ndogo kuweza kuwakabili wahalifu.
“Ukiangalia kwenye shule hii tuna wanafunzi 87 ikiwa ni mchanganyiko wa
walemavu wenye ualibinisimu,wasiosikia na wengine hawaoni hivyo ni
hatari sana iwapo kutakuwa hakuna uzio na hawa wanatoka mikoa mbalimbali
hapa”Alisema .
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM)
Mbaraka Sadi alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uzio
kwa sababu ipo kwenye mazingira magumu kwani imezungukwa na pori ambalo
ni hatari kwao.
“Hii changamoto ni kubwa sana na hatari kwa usalama wa wanafunzi
wanaosoma kwenye shule hiyo hivyo niwaombe wadau wa elimu,viongozi na
serikali kuona namna ya kusaidia jambo hilo kwa maendeleo ya taalumu za
watoto hao “Alisema.
Hata hivyo alisema pia suala la uhaba wa madarasa kwenye shule hiyo
atalichukua na kulifikisha kwenye kikao cha baraza la madiwani ili
waweze kuona namna ya kuyashughulikia.
Naye kwa upande wake,Mwenyekiti wa Mtaa wa Pongwe,Hemed Kileo alisema
kukosekana kwa uzito kwenye shule hiyo ni jambo la hatari hivyo kuziomba
mamlaka husika kuona namna ya kulishughulikia.
Alisema shule hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1948 ikiwa na darasa la
kwanza mpaka la sita ambayo walikuwa wakisoma wakoloni kabla ya mwaka
1957 kubadilishwa matumizi na kuwa shule ya bweni na baadae ikiwa ni ya
mchanganyiko .
Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha.
Comments
Post a Comment