- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Nimeona
mitandaoni kampeni inaendelea kutuhamasisha watu tusitumie mtandao wa
Vodacom.
Kampeni
inasimamiwa na kusambazwa na viongozi na wananchama wa Chama kimoja cha siasa.
Wengine ni
wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wanajenga
hoja, na kwa kweli hoja wanayo.
Wanasema
mtandao huo umeamua kutoa siri za wateja wao ili kusaidia upande wa washitaki
wanaomshtaki mbunge na mwanachama wao.
Wanaendelea
kusisitiza kwamba tuukatae mtandao huo kwa kuwa Leo wao kesho mimi na wewe.
WANASAHAU HARAKA SANA.
Mwaka 2011
mwezi Mei wakati nashiriki siasa na nikiwa Mwanachama wa Chadema.
Tukiwa
katika uchaguzi wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kupitia Vijana (Bavicha). Mimi
nilikuwa miongoni mwa wagombea wa uenyekiti wa Taifa wa Vijana.
Pamoja na
kwamba nilikuwa na nguvu za ushawishi kiasi cha kushinda. Niliitwa kujieleza katika kikao cha uchujaji
wagombea saa saba kasoro dakika 5 usiku.
Nikaenda
katika kikao hicho Mbezi Garden Hotel Iliyoko Mbezi.
Pamoja na
mambo mengine nilikuta nimetuhumiwa kwa makosa zaidi ya saba kwamba siwezi na
sistahili kugombea nafasi Ile ya uenyekiti wa Vijana.
Shitaka
langu namba Sita lilikuwa ni kutoa rushwa kwa njia ya simu kupitia M-Pesa.
Godbless
Lema alikwenda Vodacom, akaprint muamala wangu wa Vodacom wakachukua
mawasiliano yangu yote ya kifedha mpaka niliyowarushia ndugu zangu, rafiki
zangu na wazee wangu wakasema niliwatumia pesa wajumbe wa Bavicha.
Wakamuandaa
na kijana mmoja aliyeniomba nimkopeshe nauli ili ashiriki mkutano na kwamba
akirudishiwa na Chama angenilipa kumbe ulikuwa mtego wakanituhumu nimetoa
rushwa.
Wakati
John Mrema akisoma miamala yangu katika kikao cha Kamati Kuu, Mbunge Peter Msigwa alikuwa anarekodi kwa
kutumia IPad yake. (Siwezi kulisahau hili tukio maisha yangu yote).
God bless Lema
akawa shujaa kwenye hili. Kwamba aliweza kuingilia mawasiliano yangu.
Vodacom hawakuwa
wabaya hapa. Walisifiwa eti wamefichua
njama za rushwa.
Hapa
hawakujali kwamba mimi naye ni Binaadam na Nina privacy zangu.
Siku mbili
baadaye 30.05.2011 Mwandishi Alfred Lucas wa
Gazeti pendwa la MWANAHALISI likaandika MASALIA YA ZITTO YAPUKUTISHWA
CHADEMA.
Gazeti la Mwanahalisi likachapisha miamala
yangu yote waliyoiibua kwa rafiki yao aliyekuwa kigogo wa Vodacom.
Mtandao wa
Jamiiforums
nako wiki nzima habari ikawa miamala yangu ya Vodacom.
Bahati
mbaya Sana Siku zinakimbia mno.
Leo LEMA
aliyeprint Mawasiliano yangu kunikomesha naye wameprint yake na yuko matatani.
Msigwa
aliyekuwa anashangilia na kurekodi kwenye IPad yake naye analalamika
mawasiliano ya Lema kuingiliwa.
Pamoja na
kwamba siungi mkono manyanyaso ya kisheria anayokutana nayo Lema, lakini ni
vyema vijana kujifunza kuacha kukurupuka na kulalama hovyo bila kujua msingi wa
jambo.
Leo
tunajifunza kuwa kuna vitu vinaumiza vikitokea hasa vikitokea kwa upande wetu.
Maumivu
niliyoyapata mimi Mwaka 2011 wanaoweza kusema japo kwa uchache ni Godwin
Makomba na Emanuel Kidenya.
Rafiki na kaka
yangu Zitto Kabwe alitumia nguvu kubwa kunitia moyo na kunishawishi nisikishtaki Chama changu na
Vodacom. Alinitia moyo kuwa "there
is always next battle".
Wakili
Peter Kibatala nilimshirikisha sana tuwashtaki Vodacom lakini alikuwa ananipiga
chenga, kumbe alikuwa anajiandaa kuwa mwanachama hai.
Leo miaka
6 baadaye nikiwa si mwanachama wa chama chochote cha siasa yamewatokea
yaliyonitokea.
Nawakumbusha
Lema na Msigwa kuwa USILOPENDA KUFANYIWA KAMWE USIMFANYIE MWENZAKO.
Ndimi
Habib Mchange
Mwananchi
Comments
Post a Comment