- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi,
akitoa hotuba ya mafanikio ambayo Benki yake imeyapata katika biashara
ya Sekta ya Fedha ikiwemo kukuza mtaji, kupata faida na kufanikiwa
kubuni Jina Jipya na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kutumika kuanzia
leo Januari 19,2017, baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akitoa hotuba kabla ya
kuzindua rasmi Jina Jipya na Nembo vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki
ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), kuanzia Januari 19, 2017. Tukio
lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
Jijini Dar es salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akibonyeza kitufe
kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Jina Jipya na Nembo Mpya yenye alama ya
Kipepeo, (Tpb Bank Plc) vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta
Tanzania Plc, kuanzia Januari 19, 2017. Tukio lililofanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (katikati), Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Prof. Lettice Rutashobya na Mtendaji
Mkuu wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi, wakiangalia Jina Jipya na
Nembo Mpya iliyobuniwa na Benki hiyo baada ya kuizindua rasmi Januari
19, 2017, Tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (wa pili kulia),
akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw.
Sabasaba Moshingi, kwa kazi nzuri ambayo benki hiyo imefanya kubuni
Jina na Nembo Mpya itakayoanza kuitambulisha Benki hiyo katika biashara
ya Sekta ya Fedha kuanzia Januari 19, 2017, tukio lililofanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (aliyeketi kulia),
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tpb Bank Plc, Prof. Lettice
Rutashobya (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa
Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Khamis Juma, wakisikiliza kwa
makini hotuba ama wasilisho la Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Sabasaba
Moshingi, (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Jina na
Nembo Mpya itakayoanza kuitambulisha Benki hiyo katika biashara ya Sekta
ya Fedha kuanzia Januari 19, 2017, tukio lililofanyika katika ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tpb Bank Plc, Prof. Lettice Rutashobya
(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Mpango, zawadi ya saa yenye Jina na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza
kuitambulisha rasmi Benki hiyo ndani na nje ya nchi baada ya kuzinduliwa
rasmi kwa matumizi ya vitu hivyo, Januari 19, 2017, tukio lililofanyika
katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es
salaam
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tpb Bank Plc, Prof. Lettice Rutashobya
(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Mpango, kadi ya benki hiyo mara baada ya kuzinduliwa kwa Jina na Nembo
Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kuitambulisha rasmi Benki hiyo ndani na nje
ya nchi kuanzia Januari 19, 2017, Tukio lililofanyika katika ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam,
ambapo tukio la uzinduzi wa Jina na Nembo Mpya ya Benki ya Posta
Tanzania (Tpb Bank Plc) limefanyika.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango, (wa pili kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta
Tanzania (Tpb Bank Plc), Prof Lettice Rutashobya, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Fedha na Mipango wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Khamis
Juma, (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Sabasaba
Moshingi (kulia), na Baadhi ya Watendaji wakuu wa Benki hiyo, baada ya
kuzinduliwa rasmi kwa Jina na Nembo Mpya ya Benki hiyo, Katika Ukumbi wa
Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Januari 19, 2017
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango, (wa pili kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta
Tanzania (Tpb Bank Plc), Prof Lettice Rutashobya, (wa tatu kushoto),
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Serkali ya Mapinduzi
Zanzibar Bw. Ally Khamis Juma, (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa
Benki hiyo Bw. Sabasaba Moshingi (kulia), na baadhi ya wafanyakazi wa
Benki hiyo, baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Jina na Nembo Mpya ya Benki
hiyo, Katika Ukumbi wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Januari 19,
2017
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango, (wa pili kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta
Tanzania (Tpb Bank Plc), Prof Lettice Rutashobya, Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (wa kwanza kushoto),
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw, Sabasaba Moshingi (kulia), wakiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wanawake wa Benki hiyo baada ya
kuzinduliwa rasmi kwa Jina na Nembo Mpya ya Benki hiyo, Katika Ukumbi wa
Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Januari 19, 2017
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Comments
Post a Comment