- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
DK. KIGWANGALLA ATOA SIKU 7 KWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA KUMALIZA CHANGAMOTO ZINAZOIKUMBA HOSPITALI YA RUFAA YA KITETE
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia , Wazee na watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku siku 7
kwa Katibu Mkuu kumaliza changamoto zinazoikumba hospitali ya Rufaa ya
Kitete iliyopo mkoani Tabora.
Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo
alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Rufaa ya Kitete
Mkoani Tabora na kukagua miradi ya chumba cha upasuaji pamoja na
Chuo cha AMOS kilichopo mkoani humo.
“Chumba hiki cha upasuaji na
Chuo vimekamilika mpaka thamani za ndani tangu miaka miwili iliyopita
Sababu ni kwamba Serikali yetu haikutoa counter-part funding huku Benki ya
Maendeleo ya Afrika ikiwa imetimiza ahadi yake kwa asilimia mia
moja”alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo Dkt. Kigwangalla amesema
kuwa amefurahishwa kutekelezwa kwa baadhi ya maagizo aliyoyatoa kama vile
kuondoa msongamano wa wagonjwa kwenye wodi za wanawake wajawazito na
watoto.
Kwa mujibu wa Dkt. Kigwangalla
amesema kuwa uongozi wa Hospitali hiyo umefanikiwa kuboresha huduma ya
upatikanaji wa dawa zote muhimu na huduma kwa wateja ikiwemo lugha nzuri
kutoka kwa wahudumu imeboreshwa..
Aidha Dkt. Kigwangalla amesema
anashukuru uongozi wa Hospitali hiyo kwa kufanya ukarabati mkubwa wa majengo ya
wodi za wagonjwa na sasa hakuna tena msongamano na huduma zinatoka kwa wakati sahihi.
Comments
Post a Comment