- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea bajeti mbalimbali za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo(picha na woinde Shizza wa libeneke la kaskazini Arusha)
Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiwa anahubiri katika
hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha hii leo
Nabii mkuu akiwa anaendelea na huduma ya sikuu kuu ya kukusanya hii leo
Nabii akiwa anamwaga upako kwa waumi waliouthuria katika siku kuuu hii ya kukusanya hii leo (picha na Woinde Shizza,Arusha )
Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea bajeti mbalimbali za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo
Habari picha na woinde shizza,Arusha
Watumishi wa madhehebu mbalimbali hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kuwasaidia yatima ili nao waweze kujisikia kama wao ni sehemu ya jamii
Hayo yamebainishwa leo na Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie wakati akifanya dua maalumu ya kupitisha bajeti ya watu walioshiriki katika sikukuu ya kukusanya iliyofanyika katika hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha.
Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtumishi kukusanya na kutoa kile alichonauwezo nacho ili kuweza kuwasaidia watoto yatima ,wananchi wasiojiweza ili kuweza kuwafanya nao wajisikie ni sehemu ya jamii
Alisema kuwa mbali na watoto yatima pia aliwasihi makanisa ambayo yanajiweza kuweza kusaidia yale ambayo ni machanga ili kuweza kuwapa nguvu ya kuweza kuendelea kueneza injili na kumtangaza mungu kupitia makanisa yao .
Nabii mkuu Dr Geordavie alisema kuwa kuwa lengo la sikukuu hii ya kukusanya nikuwasaidia watoto yatima kwa kuwapa chakula kama mchele, sukari pamoja na mafuta yakupikia ili nao wajisikie wanafuraha haswa katika kipindi hichi cha sikukuu.
Alisema kuwa licha ya misaada hiyo kwenda kwa watoto yatima, pia atatoa fedha kwa watumishi wa mungu wenye makanisa madogo hapa nchini lengo likiwa ni kuinua huduma zao na kuwasaidia katika kuendeleza huduma zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kanisa, ununuzi wa vyombo vya muziki na shughuli nyingine za kanisa.
Sikukuu hii ya kukusanya huadhimishwa na huduma ya Ngurumo ya Upako Duniani tarehe 26 ya kila mwaka, watu hutoa sadaka ya vitu mbalimbali ikiwemo fedha kwa mujibu wa maelekezo ya Nabii Mkuu na kisha hugawanywa kwa vituo vya watoto yatima huku fedha zikigawanywa kwa watumishi waliotuma maombi ya kupata msaada wa kuendeleza huduma zao.
Mwaka jana msaada wa zaidi ya shilingi milioni 15 ulitolewa na waumini wa kanisa la Ngurumo ya upako na kugawanywa katika vituo mbalimbali vya watoto yatima huku fedha zikigawiwa kwa baadhi ya makanisa madogo kwa ajili ya kuwasaidia mambo mbalimbali .
Comments
Post a Comment