- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Shavkat Berdiev (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kampuni hiyo kutangaza ofa ya Krismas ya Smartphone. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imetangaza kuzindua ofa mpya ya Tecno Y3+ Music Smartphone ambayo imejengewa ndani yake zana kubwa ya kuchezesha ambayo inatoa nafasi ya kutiririsha kupitia mtandao na hivyo kuwawezesha wateja kufurahia na kusherehekea na wapendwa wao wakati wa kipindi hiki cha kipekee kinachohusiana na Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Akitangaza ofa hiyo katika mkutano wa waandishi wa habrai jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigom, Shavkat Berdiev alisema kuwa Simu ya mpya ya kisasa ya Smartphone tayari ipo katika maduka yote ya Tigo na mawakala nchi nzima na inapatikana kwa gharama ya shilingi 99,999 tu. Hii ni aina ya kwanza ya simu ya kisasa ya Techno Smartphone kuingizwa katika soko ikiwa na zana kubwa (Boom App) ilibeba miziki ya ndani.
“Tunaamini ofa hii itawawezesha wateja wengi wa Tigo kufurahia manufaa ya simu hii ya kisasa inayouzwa kwa bei ya reja reja ambayo mteja anaimudu, ikiwemo kupata mtandao wa intaneti ambao uko pamoja na kujikita kwetu katika kuboresha mabadiliko katika maisha ya kidijitali,’ alisema Berdiev.
Aliongeza, “Hali kadhalika imekuwa ni utamaduni wetu kuwapatia wateja simu nzuri ya kisasa wakati wa msimu wa sikukuu. Hivyo natoa wito kwa wateja wetu wote hususani wale wanaosafiri kwenda mikoani hadi maeneo ya vijijini kuungana na familia zao kuchukulia faida ya kuwepo kwa ofa hii.”
Akizungumza katika tukio hilo Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga aliongeza;Pindi mteja anaponunua simu, moja kwa moja Tigo inamzawadia mteja huyo GB 1 ya data za intaneti na muda wa maongezi shilling 5,000 Tigo kwenda Tigo kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja (miezi 12).
Simu ya Kisasa ya Y3+ imekuja na vitu mahsusi vya kipekee ambavyo vinajumuisha betri iliyoboreshwa maisha, sehemu mbili za kadi za simu, uwezo wa kuhifadhi data kwa kiwango cha GB 8 pamoja na kasi ya ufanisi 512 (RAM) ambazo zinaifanya kuendesha na kuhifadhi data.
Comments
Post a Comment