- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
SIMBACHAWENE AAGIZA FEDHA ZILIZOTOLEWA KWA KAYA ZISIZOKUWA NA SIFA KATIKA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI KUREJESHWA.
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Rebecca Kwandu,
Dodoma
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George
Simbachawene ameziagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi
wa Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa kwa
kaya zisizokuwa na sifa katika Mpango wa kunusuru kaya maskini unaofanywa kwa
uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) kurejeshwa ili ziweze kuwanufaisha walengwa.
Mhe.
Simbachawene pia amewaagiza Wakurugenzi
wa Halmashauri kuwasimamisha kazi Waratibu wote wa TASAF wilaya ili kufanya
uchunguzi wa jinsi walivyojihusisha katika kuvuruga utekelezaji wa Mpango wa
kunusuru kaya maskini kwa kuandikisha kaya zisizokuwa na sifa na ametaka wale
wote watakaobainika kuhusika katika kutenda makosa mamlaka za kinidhamu
kuchukua hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mhe. Simbachawene
amesema usimamizi dhaifu wa mpango wa TASAF katika ngazi za halmashauri
hususani Waratibu wa Mpango wa TASAF Wilaya wasiokuwa waaminifu katika
kutekeleza majukumu yao imesababisha fedha za Mpango wa TASAF kutumiwa na watu
wasiokuwa walengwa.
Waziri
Simbachawene pia amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuwachukulia hatua
watumishi wa ngazi za Kata, Mitaa na Vijiji ambao kwa namna moja au nyingine watabainika
kuhusika katika kuvuruga Mpango wa kuzinusuru kaya maskini kuchukuliwa hatua za
kinidhamu.
Aidha,
Mhe. Simbachawene amewataka Wakuu wa Mikoa kujiridhisha katika mikoa yao ikiwa
Wakurugenzi watachukua hatua stahiki dhidi ya watumishi wasiokuwa waaminifu na
kuwataka kumpelekea taarifa hiyo ndani ya siku kumi na nne kuanzia leo tarehe
25/11/2016.
Mheshimiwa
Simbachawene ameitaja mikoa inayoongoza kwa matumizi mabaya ya fedha za Mpango
wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF kuwa ni Dar es Salaam,
Kilimanjaro, Morogoro, , Shinyanga, Arusha, Kigoma, Dodoma, Arusha na Mbeya.
Comments
Post a Comment