- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais Dk. John Magufuli
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dk. John Magufuli,
amepiga marufuku uuza uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na
kutaka wale wote wanaouza wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.
Taarifa
iliyotolea kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Naibu Mkurugenzi wa
Mawasiliano Ikulu, Jaffar Haniu ilisema Rais Dk. Magufuli alifia uamuzi huo
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga,Dar es Salaam.
Taarifa
hiyo, ilisema Rais Dk. Magufuli amepiga marufuku hiyo kutokana na maelezo ya
baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi
hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi.
Kutokana
na hali hiyo, Rais Dk. Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama
kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare hizo.
”Haiwezekani
sare za majeshi yetu kuuzwa na watu binafsi hili haliwezekani kamwe, labda
baada ya kumaliza muda wangu,” alisema Rais Dk. Magufuli”
Pia
amepiga marufuku majeshi yote kuingia
ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya
biashara na kutaka maeneo ya majeshi yabaki katika jeshi husika.
Katika
hatua nyingine, Rais Dk. Magufuli ametoa Sh bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza
kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari
wake katika Gereza la Ukonga.
Hatua hiyo
inatokana na kilio cha askari Magereza, kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi
uraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi hata kuzorotesha utendaji kazi wao wa kila
siku.
Taraifa
hiyo, iliongeza kuwa ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika
ipasavyo katika uzalishaji mali, badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi wamekuwa
wakitumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.
Aliwahakikishia maofisa na askari wa jeshi hilo kuwa Serikali itaendelea kuboresha
maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine.
CHANZO -
MTANZANIA
Comments
Post a Comment