- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
By Habel Chidawali, Mwananchi
Dodoma. Wateja wakiwamo wawekezaji kutoka nje wameamua
kuyakimbia machinjio mjini Dodoma na kuhamia mitaani kufanya shughuli hiyo.
Machinjio
hayo yanayomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali yenye hisa asilimia 49 na mwekezaji
anayemiliki hisa asilimia 51, yalikuwa yakitumiwa na wawekezaji 13 wanaochinja
na kusafirisha nyama nje lakini sasa wamebaki wawili.
Idadi ya
mifugo inayochinjwa hapo pia imepungua kutoka mbuzi 1,200 kwa siku hadi 500,
huku idadi ya ng’ombe ikipungua kutoka wastani wa 200 kwa siku hadi 30.
Chanzo cha
kukimbia wateja na wawekezaji kimetajwa kuwa ni utitiri wa kodi zinazotozwa na
Serikali kwa watu wanaochinja na kusafirisha nyama nje na hata watumiaji wa
ndani.
Uzalishaji
wa machinjio hayo, Hamisi Kissoyi amesema kuwa hali ni mbaya hivyo wameamua
kupunguza wafanyakazi kutokana na uchumi kuyumba jambo lililosababisha idadi ya wateja
kuwakimbilia.
Amezitaja
kodi zinazotozwa kwa mtu aliyenunua mfugo akitaka kusafirisha nyama ni ya awali
mnadani (primary), kodi ya kwenye soko (secondary), machinjio, ya wizara, Bodi ya Nyama na ya usafirishaji.
Mfanyabiashara
wa bucha ya nyama mjini Dodoma, Andrew Bogobo amesema hawezi kupeleka ng’ombe
kwenye machinjio hayo kutokana na gharama zinazotozwa kuwa kubwa.
CHANZO -
MWANANCHI
Comments
Post a Comment