- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri Ofisi
ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah
Possi akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali
halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es salaam.
Wageni waalikwa wakimsikiliza
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu
Dkt. Abdallah Possi wakati wa uzinduzi wa
taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee
nchini jijini Dar es salaam.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) Bakar Fakih
akiwasilisha taarifa ya utafiti waliofanya kuhusu maisha ya wazee na watu wenye
ulemavu ambao umebainisha kuwa bado kuna imani potofu kwenye jamii juu ya wazee
na watu wenye ulemavu.
Mshiriki Rika (kundi la wazee) Bi. Elizabeth Nkwera akichangia
juu ya utafiti waliofanya wakati wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye
mahitaji maalum walipowasilisha matokeo ya tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali
Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini.
Mshauri Maendeleo ya kijamii kutoka Uingereza Idara ya Maendeleo
ya Kimataifa Isabelle Abbott Pugh akitoa mchango wake kuhusu dhana ya kuwajali
watu wenye ulemavu na wazee wakati wa uzinduzi wa taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali
halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na wazee mara baada ya uzinduzi wa
taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee
nchini jijini Dar es salaam, wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Sightsavers
nchini Gosbert Katunzi. Wa kwanza kulia ni Bi. Clotilda Isdori Kokupima kutoka
wilaya yak ASULU mkoani Kigoma na katikati ni Bw. Elisha Sibale kutoka
halamashauri ya Kibaha mkoani Pwani.
Wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum wakimsikiliza
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu
Dkt. Abdallah Possi mara baada ya uzinduzi wa utafiti Mpya wa Ubainishaji Hali
Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini.
Mwakilishi wa Sightsavers nchini Gosbert Katunzi
akiongoza mjadala wakati wa uzinduzi wa taarifa mpya ya utafiti inayobainisha
hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na
Eleuteri Mangi, MAELEZO
Watafiti
wa masuala mbalimbali ya kijamii nchini wametakiwa kuhakikisha wanafanya tafiti
ambazo zitawasaidia watu wenye ulemavu kupata vifaa saidizi ili waweze kumudu
kuendesha maisha yao ya kila siku.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na
Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi alipokuwa akizindua taarifa mpya ya
utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es
salaam.
“Serikali
inafarijika inapoona watu wanafanya utafiti ili kuwasaidia watu wenye ulemavu
waweze kupata vifaa saidizi na ni kitu gani kifanyike ili NGOs ziweze
kujikwamua kiuchumi na kuwasaidia wenye mahitaji” alisema Dkt. Possi.
Kuhusu
suala la unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu, Dkt. Possi amesema kuwa Ofisi ya
Waziri Mkuu hapo tayari kuona wananchi wananyanyapaliwa huku akisisitiza kuwa
watu wote ni sawa na ofisi hiyo ina “zero tolerance” kwa watu wanaowanyayapaa
mlemavu.
Katika
masuala ya kisheria kwa watu wenye ulemavu, Dkt. Possi amesema kuwa inapotokea
mlemavu au mzee amefanyiwa kosa taarifa itolewe mara moja ili hatua za kisheria
zichukuliwe dhidi ya waliofanya makosa hayo na haki iweze kutendeka.
Naibu
Waziri Dkt. Possi pia amezitaka Asasi zinazoshughulika na watu walemavu wafanye
kazi kwa pamoja ili kuwasaidia walengwa ambao ni walemavu, watoto na wazee na
kuwataka kutumia fursa waliyonayo ya kupata msaada kisheria bure kutoka kwenye
taasisi za sheria ikiwemo Chama cha Mawakili (Tanganyika Law Society), TAMWA
pamoja na taasisi nyingine za kisheria
wakati masuala ya jianai amewataka wayapeleke kwenye polisi kwa hatua zaidi za
kisheria huku akisisitiza kumshirikisha inapobidi kufanya hivyo.
Akitoa
maelezo ya utafiti huo wakati wa uzinduzi, Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya
Ifakara (IHI) Bakar Fakih amesema kuwa utafiti huo umewashirikisha watafiti
rika mbalimbali wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu na kubainisha kuwa bado
kuna imani potofu kwenye jamii juu ya wazee na watu wenye ulemavu.
Utafiti
huo unaoongozwa na kaulimbiu “Ulemavu na uzee sio laana” umebainisha kuwa watu
wenye ulemavu na wazee nchini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
kupata elimu, huduma za afya, unayanyasaji wa kingono na kuvunjika kwa ndoa,
kutokujaliwa na familia pamoja na kutengwa kwa watu wenye ualbino kutokana na
mila potofu.
Kwa
upande wake mtafiti rika Blandina Isaya amesema kuwa walemavu waachwe wafanye
maamuzi yanayohusu maisha yao ikiwemo masuala ya ndoa wawe huru kuchagua wenza
wao badala ya kuchaguliwa na familia zao kwa kuwa wanahaki kama watu wengine
wasio na ulemavu.
Katika
kuhakikisha familia zinakuwa imara kiuchumi, Blandina amesema kuwa familia
zenye watu wenye ulemavu na wazee wapewe elimu ya ujasiriamali ili waweze kuwa
na uwezo wa kuendesha maisha yao kwa kulea familia ipasavyo na kuomba Seriklai
za mtaa ziwe na takwimu za wazee na watu wenye ulemavu.











Comments
Post a Comment