- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
SERIKALI, MASHIRIKA YA KIMATAIFA YAWEKA MIKAKATI YA KUWASAIDIA NA KUWALINDA WATOTO WALIOATHIRIKA NA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WA BINADAMU NCHINI
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu
wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (wapili kulia-meza
kuu), akitoa hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya Siku mbili ya kujadili jinsi ya
kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha
binadamu. Fella alisema wadau wa warsha hiyo watatoa elimu kwa umma jinsi ya
kuwasaidia idadi kubwa ya watoto ambao wameathirika. Wapili kushoto meza kuu ni
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki
kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa
la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi, na kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika
la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Tamara Keating. Warsha hiyo inafanyika katika
Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Mwakilishi
Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla,
Balozi Roeland Van de Geer akitoa hotuba yake katika Warsha ya siku mbili ya
kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya
kusafirisha binadamu nchini. Katikati ni Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya
Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Separatus Fella, na kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Kimataifa
la Uhamiaji (IOM), Tamara Keating. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya
Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (katikati), akiteta
jambo na Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika
Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer, mara baada ya Katibu huyo
kufungua Warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia
watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu nchini. Fella alisema
baada ya warsha hiyo, washiriki hao wataanza kutoa elimu kwa umma jinsi ya
kuwasaidia idadi kubwa ya watoto ambao wameathirika. Kushoto ni Mkuu wa Shirika
la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi. Warsha hiyo inafanyika
katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Katibu
wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (wapili
kulia-waliokaa), Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na
Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer (wapili kushoto-waliokaa),
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi
(kushoto-waliokaa), Meneja wa Mradi Umoja wa Ulaya (EU), Anna Costantini,
wakiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka Taasisi za Serikali pamoja na
Mashirika yasiyokuwa ya Serikali, mara baada ya kufunguliwa warsha ya siku
mbili ya kujadili namna ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na
biashara ya kusafirisha binadamu nchini. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli
ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Na Felix
Mwagara, MOHA
SERIKALI
kwa kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa wameanza kujadili nyenzo mbalimbali
ambazo zitasaidia kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya
kusafirisha binadamu nchini.
Akizungumza
wakati akifungua warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na
kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu,
inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam leo, Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na
Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus
Fella alisema warsha hiyo ni muhimu ikiwa na lengo la kusaidia idadi kubwa ya
watoto walioathirika nchini.
Alisema Tanzania
ambayo ni kati ya mataifa yanayoshamiri kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto
kwa lengo la kwenda kuwatumikisha kazi katika maeneo mbalimbali nchini pamoja
na duniani kwa ujumla, kupitia nyenzo hizo zitakazo jadiliwa zitasaidia kutoa elimu kwa umma juu ya matatizo hayo
nchini.
“Nyenzo
hizi za kuwasaidia na kuwalinda wale watoto walioathirika baada ya kutoka
katika maeneo mbalimbali zitasaidia kutoa elimu ya kuwandaa kisaikolojia ili
wasikate tamaa na maisha, pia watoto watalindwa na baadaye watarudishwa kwa
wazazi wao ili waweze kuendelea majukumu mengine ya kujenga taifa,” alisema
Fella na kuongeza;
“Kumekuwepo
na wimbi kubwa la kuwasafirisha wasichana wa Kitanzania kwenda nchi za uarabuni
kwa lengo la kwenda kufanya kazi za ndani, ila wanapofika huko mambo
yanawaharibikia wanaanza kudhalilishwa,
kunyanyaswa kiasi kwamba wanashindwa kupata misaada, kutokana na manyanyaso
hayo urudi nchini wakiwa wameathirika kwa kiasi kikubwa.”
Fella
alisema wadau wa warsha hiyo watatoa elimu kwa umma kuhusu kukomeshwa kwa
biashara hiyo haramu na wazazi kutokuwaruhusu watoto wao kwenda kufanyiwa
unyanyasaji huo kwa kuwa ni kinyume cha sheria. Hata hivyo, kutokana na wimbi
hilo kuzidi kushika kasi nchini, pia wadau hao watatoa elimu ya watoto
walioathirika mara baada ya kurudi nchini ili wajitambue kutokana na mateso
mbalimbali waliokumbana nayo ili wasiweze kukata tama kutokana na vitendo vya
ukatili walivyofanyiwa katika maeneo wanayotoka.
Aidha,
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki
kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer alisema Tanzania ni kati ya nchi
zilizoathirika na biashara haramu ya kusafirisha watoto, hivyo elimu inahitajika
ili kukomesha biashara hii hatari.
“Watoto wa
leo ni mabibi na mabwana wa kesho, hivyo wapaswa kulindwa pamoja na
kuelimishwa, Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika
kuwasaidia watoto waweze kuepuka mateso wanayoyapata,” alisema Roeland.
Warsha
hiyo iliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kufadhiliwa na Umoja wa
Ulaya pamoja na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na inatarajiwa
kumalizika Oktoba 20 mwezi huu ambapo wadau hao wataanza kufanyia kazi nyenzo
hizo zilizojadiliwa.
Comments
Post a Comment