- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
UKUTA uliokuwa usimamishwe na Chadema kwa maandamano ya nchi nzima Septemba Mosi, mwaka huu umeporomoka baada ya viongozi wakuu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe, na aliyekuwa mgombea urais Edward Lowassa kutakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam Alhamisi, siku ambayo walipanga kuandamana.
Hali hiyo inafuatia kukamatwa kwa viongozi hao leo mchana na kuachiwa kwa dhamana kwa viongozi watano waandamizi wa Chadema wakiwemo Mbowe na Lowassa.
Ili kuepuka mgongano na sheria, viongozi hao watapaswa kuripoti polisi badala ya kuratibu na kusimamia Ukuta.
Wakati viongozi hao wanakamatwa, naye Mbunge wa Chadema wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amechiliwa na polisi baada ya kushikiliwa kwa siku tatu.

Comments
Post a Comment