Jambo hili limemsukuma Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturukufanya ziara na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo kwa lengo la kuwaelemisha juu ya uvunjaji sheria za nchi kwa kuendelea kusalia katika maeneo ambao wametakiwa kuhama jambo ambalo kama watashindwa kulitekeleza serikali itawatoa kwa nguvu kwani kwa kiasi kikubwa wanaharibu mazingira.
Akizungumza na Wananchi hao katika Kijiji cha Kaugeri Kata ya Mwaru Wilayani hapa Dc Mtaturu ametoa mwezi mmoja kwa wananchi hao kuhama haraka iwezekanavyo ili kupisha eneo hilo la Hifadhi ya msitu kufanya Kazi iliyokusudiwa kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Mtaturu amesema kuwa Kwa mujibu wa sheria Kijiji kinapaswa kutoa Ardhi hekari zisizozidi hamsini kwa mwekezaji lakini uongozi wa Kijiji hicho umegawa kwa mwekezaji hekta 150 hadi 200 kinyume kabisa na taratibu za kiutendaji ukiwa ni pamoja na kuingia mikataba ya kinyonyaji.
Pamoja na hayo pia viongozi hao wametoa Ardhi hiyo bila kushirikisha wananchi jambo ambalo limeibua hisia Kali kwa wananchi ambao wanatambua uporwaji huo wa maeneo yao.
Kufuatia kadhia hiyo ya viongozi hao kugawaji Ardhi kinyume na taratibu Dc Mtaturuamewaweka lumande Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri Mange Nkuba, Aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Laurent Bomba, na mjumbe wa serikali ya Kijiji Paul Kilo huku Amani Clement ambaye alitoweka kabla Ya mkutano kumalizika anaendelea kutafutwa mpaka apatikane.
Katika hatua nyingine Dc Mtaturu ameagiza mkandarasi Samwel John kukamatwa na kuhojiwa kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji tangu Mwaka 2013 ambapo tayari alishapewa kitita cha shilingi milioni 19 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
Hata hivyo pamoja na mkandarasi kukabidhiwa fedha hizo alianza ujenzi lakini jengo hilo halijafika hata kwenye Renta huku likiwa limejengwa chini kiwango.
Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi amemuagiza mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya hiyo kupitia idara ya ujenzi kutoa taarifa kwanini hawakushiriki kutoa huduma za kiutaalamu katika kusimamia jengo hilo la umma kabla na wakati ujenzi unaanza.
Comments
Post a Comment