Hillary Clinton
Maafisa wa upelelezi nchini Marekani
wamesema kuwa programu ya komputa inayotumiwa na jopo linalosimamia
kampeni ya Bi Hillary Clinton imedukuliwa.
Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta hiyo.
Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.
Vyombo vya habari Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.
Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa
linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha
udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.
Juma
lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa
kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana
na chama cha Democratic.
BBC/SWAHILI
Comments
Post a Comment