Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
amewaambia maseneta wa Marekani waliozuru taifa hilo kwamba watajutia
kutofanya urafiki naye iwapo Donald Trump atachaguliwa kuwa rais katika
uchaguzi wa mwezi Novemba.
Maseneta hao Chris Coons na Adam Schiff
waliambia gazeti la Politico nchini Marekani kwamba walikuwa katika
taifa hilo kuzungumzia kuhusu usafirishaji wa wanyama mwitu na kwamba
waliomba kukutana na rais huyo na wakashangaa kwamba alikubali kuonana
nao.
Maseneta hao wamesema kuwa Mugabe aliwataka kuelezea kwa nini
Marekani inaliwekea vikwazo taifa hilo ambapo walitoa sababu kadhaa.
Ni wakati huo ambapo bwana Mugabe aliwaambia: ''Wakati Trump atakapokuwa rais mutatamani mungefanya urafiki nami''.
BBC/SWAHILI
Comments
Post a Comment