- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Hii ndio CV ya mbunge Agness Marwa aliyesema kuwa anasikia uchungu sana bunge kuoneshwa Live. Akiwasilisha mchango wake bungeni alisema anasikia uchungu mno bunge kuoneshwa Live kiasi kwamba anatamani kulia. Hataki kabisa wananchi watizame bunge Live.
CV yake ina maajabu yafuatayo;
#Ajabu Namba Moja
Agness amesoma shule mbili za sekondari kwa wakati mmoja. Nyaibara Secondary na Kenton High School. Mwaka 2009 alifanya mtihani kama QT Nyaibara uliomuwezesha kufanya mtihani mwaka 2010 kama school candidate ambapo alifanikiwa kupata alama 32. Kipindi hichohicho kati ya 2008 hadi 2014 alikua Kenton High School ambapo alihitimu na kufanikiwa kupata alama za juu zaidi yani Div.4 ya pointi 33.

#Ajabu Namba Mbili
Agness amezaliwa mwaka 1978 lakini ameanza form one mwaka 2008 akiwa na miaka 31. Tena sio elimu ya watu wazima. Hasha! Elimu ya kawaida ya kuvaa sketi na blauzi nyeupe na kuchapwa viboko. Kidumu Chama cha Mapinduzi.

#Ajabu Namba Tatu
Agness akiwa kidato cha pili mwaka 2009 alidahiliwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kampasi ya Mlimani ambapo alipata fursa ya kusomea taaluma ya Teknolojia ya Habari na mawasiliano kabla ya kurudi tena shuleni Kenton kuendelea kidato cha pili.

#Ajabu Namba Nne
Agness amesoma Elimu ya Sekondari miaka 6 akishindwa kufaulu licha ya kutokuwa na mchujo. Mwaka 2009 akiwa kidato cha pili mtihani wa mchujo wa kidato cha pili ulifutwa kwa hiyo wanafunzi wote waliendelea na kidato cha 3 hata "waliofanya vibaya". Lakini Agness alishindwa hata "kufanya vibaya" ili aendelee kidato cha 3. Hivyo akarudia kidato cha pili miaka mitatu mfululizo kabla ya kuruhusiwa kuendelea na kidato cha tatu mwaka 2013 baada ya walimu kuona anapoteza muda.

#Ajabu Namba TanoAkiwa kidato cha pili mwaka 2010 alikuwa Mkurugenzi Mtendaji (Managing Director) wa Kampuni ya Aggy Classic Enterteimnent, na alikuwa akipewa tenda kubwa za kuandaa matamasha ya Mwenge na sherehe mbalimbali za CCM.
#Ajabu Namba Sita
Akiwa kidato cha kwanza mwaka 2008 alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Watumiaji wa Mazao ya Ziwa Victoria Musoma (Sea Food Union). Kwa hiyo alikuwa anadhibiti mazao yote ya ziwani. Yani ili Professor wa pale Buhare aweze kula samaki ilikuwa lazima Agness (mwanafunzi wa kidato cha kwanza wakati huo) atoe idhini. Yeye ndiye alikuwa na ithibati ya mazao yote ya ziwani kupitia Musoma Sea Food Union.

#Ajabu Namba Saba
Akiwa kidato cha pili mwaka 2007 tayari alikuwa Mkufunzi aliyebobea (Experienced Facilitator) wa masuala ya ujasiriamali kupitia Shirika la Nyang'oto. Hii inaonesha huyu dada ni 'genius' maana watu wanasomea shahada za Ujasiriamali vyuo vikuu miaka mitatu au zaidi, lakini yeye amekuwa mkufunzi mbobevu akiwa kidato cha kwanza tu. CCM ni ileile.. oooh ni ileile.!

#Ajabu Namba Nane
Kwa miaka 14 kutoka mwaka 1994 hadi 2008 Agness alikuwa nje ya mfumo rasmi wa Elimu akikijenga chama chake. Hakika CCM ina mikakati hodari..

#Ajabu Namba Tisa
Akiwa kidato cha tatu mwaka 2013 Agness alichaguliwa kwa kishindo kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwabwaga maelfu ya wanawake wenzie walioomba nafasi hizo.

#Ajabu Namba Kumi
Pamoja na yoooote hayo Agness ni Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chombo cha juu kabisa cha maamuzi katika nchi. Na anategemewa kutoa mawazo yake yalete maendeleo kwa wananchi. Duuh bado tuna safari ndefu sana. CCM Hoyeee.!!

#MyTake
Msimamo wangu tangu kale huwa siamini katika elimu za "vyeti" lakini huyu kazidi. Japo siamini katika Elimu za vyeti but this is too much aisee. Hivi Tanzania ya viwanda inawezekana kwa wabunge wa aina hii??

Anyway sahau yote lakini usisahau "NASIKIA UCHUNGU SANA, NATAMANI HATA KULIA"
CHANZO: JAMIIFORUMS

Comments
Post a Comment