- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta
(hawapo pichani) wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo
jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada
ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa
yamechanganyika na mafuta ya petroli.
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta
wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es
salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika
baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika
na mafuta ya petroli.
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta
wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Nishati na
Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya
mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar
es salaam eneo yalipo matanki ya mafuta ya kampuni ya GAPCO ili kujionea hali
ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya
mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni wa Kampuni ya Oryx Energies Godifrey Fernandes akimuonesha Waziri wa
Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo baadhi ya maeneo yanapohifadhiwa
mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar
es salaam.
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo (wa pili mtasari wa kwanza kulia) akiongozana na baadhi
ya viongozi wa makampuni ya mafuta eneo la “Deport” ya PUMA wakati wa ziara ya
kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta katika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya madereva wanaosafirisha mafuta
ndani na nje ya nchi leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
28/05/2016
Serikali imewatoa hofu na
kuwahakikishia Watanzania na abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini kwamba mafuta
ya ndege yapo ya kutosheleza matumizi kwa muda wa siku 14 wakati shehena
nyingine za mafuta hayo zinaendelea kuingia nchini.
Hayo yamesememwa na Waziri wa
Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alipofanya ziara leo jijini Dar es
salaam kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta ili kujionea hali ya upatikanaji wa
mafuta ya ndege nchini baada ya kugundua baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa
nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
“Mafuta ya ndege yapo na ndege
zitaendelea kufanya safari kama ratiba zao zilivyopangwa na Watanzania msiwe na
wasiwasi, tumejiridhisha, mafuta yanatosheleza kwa muda wa siku 14 wakati hatua
ya shehena nyingine kuingia nchini zinaendelea” alisema Prof. Muhongo.
Ziara hiyo ya Waziri Prof. Muhongo
inafuatia kugundulika kwa mafuta ya ndege yaliyoingizwa nchini mapema mwezi Mei
mwaka huu, ambayo hayafai kwa matumizi yaliyokusudiwa kutokana na kuchanganywa
na mafuta ya petroli.
Aidha, Prof. Muhongo ameitaka
kampuni ya Sahara Energy Resources yenye makao yake makuu nchini Nigeria ambayo
ndio ilioingiza mafuta hayo nchini, kusimamisha shughuli zake mara moja hadi
suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Imeonekana si mara ya kwanza kwa
kampuni hiyo kuingiza mafuta machafu nchini, hatua iliyomfanya Waziri huyo
kuchukua msimamo huo wa Serikali hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Akizungumzia hatua hiyo na hali
ya mafuta nchini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uingizaji Mafuta kwa
Pamoja nchini, Michael Mjinja amesema kuwa mafuta ya ndege yapo na yanatosheleza
kwa wiki mbili kuanzia sasa.
Mjinja aliongeza kuwa wanakuhakikisha
uhaba wa mafuta hayo hautokei tena nchini ambapo wanaendelea kushirikiana na kampuni
ya Total na SP Rwanda ambazo hadi sasa ndio zenye mafuta safi yanayokubalika
kwa matumizi.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya TIPER iliyoko eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam,
Stephane Gay amesema kuwa kampuni yake ina nafasi ya kutosha ya kuyahifadhi
mafuta yote ambayo hayastahili kutumika ili matanki na mitambo ya kampuni zote
zilizopata mafuta hayo yafanyiwe usafi upya tayari kwa kuweka mafuta safi
yanayoingia nchini.
Ziara ya Waziri Prof. Muhongo imehusisha
kutembelea matanki ya kampuni tano za mafuta ikiwemo Puma, GAPCO, Oil Com,
TIPER pamoja na Kampuni ya Oryx Energies.
Comments
Post a Comment