Featured Post

RC MANYARA KUUNDA TUME KUTATUA MGOGORO WA ARDHI

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera

Mbulu. Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera ameahidi kuunda tume maalum, kuchunguza mgogoro wa ardhi,katika kijiji cha Eshkesh Wilayani Mbulu baina ya wananchi na Serikali ya mkoa ,baada ya Serikali kusitisha mkataba wa Mwekezaji katika kijiji hicho.

Wananchi wa kijiji cha Eshkeshi, wamesaini mkataba wa kutoa ardhi hekari 3903 kwa Mwekezaji mzawa, Geso Bajuta tangu mwaka 2010, ambaye ameanzisha mradi wa ufugaji wa kisasa na baadaye anatarajia kujenga kiwanda cha maziwa.
Akizungumza na mwananchi jana, baada ya wakazi wa kijiji hicho, kumuomba Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi, kuingilia tena kati mgogoro huo wakipinga kusitisha mkataba huo, Bendera alisema mkoa umeamua kuunda tume maalum ikayohusisha kamishna wa ardhi na wataalam wengine.
Akizungumzia mgogoro huo, Bajuta alisema mgogoro katika eneo hilo, unatengenezwa na baadhi ya viongozi wa serikali na wanasiasa kwa maslahi yao, kwani yeye hana mgogoro na wananchi kwani tayari ametimiza ahadi nyingi alizowapa wananchi.
Bajuta alisema kabla ya kumiliki eneo hilo kisheria alifuata taratibu zote, ikiwepo kufikisha suala hilo ngazi ya wilaya, Mkoa, Kamishna ardhi kanda na Ofisi ya Rais ambao waliridhia mkataba huo.

CREDIT: MWANANCHI

Comments