- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisaidia kuhesabu
vipande vya dhahabu huku akishuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi aliyevipokea kutoka kwa Waziri
wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma dhahabu pamoja na pesa
zilizokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi
zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye
hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Julai
24, 2019.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akipokea
kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma dhahabu
pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta
jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania
kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo
Jumatano Julai 24, 2019
Ndege maalum ya Jeshi la Kenya iliyobeba Dhahabu ya Tanzania
iliyokamatwa Kenya ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
atashuhudia makabidhiano hayo Ikulu Dsm kutoka kwa Mjumbe Malalum wa Rais Wa
Kenya Mhe. Uhuru Kenyata. PICHA NA IKULU
Na Waandishi Wetu
MAELEZO
DAR ES SALAAM
24.7.2019
RAIS Dkt.
John Magufuli aipongeza Serikali ya Kenya kwa maamuzi yake ya kuirejeshea
dhahabu zenye uzito wa kilo 35.34 zilizotoroshwa nchini Tanzania na
Wafanyabiashara wasio waamini kwa njia ya magendo mwaka 2018.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi dhahabu pamoja na fedha taslimu akiwa pamoja na
ujumbe wa Mawaziri na Watendaji wa Serikali ya Kenya leo Jumatano (Julai 24,
2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kitendo kilichofanywa
na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni cha kizalendo na kimedhirisha urafiki na
undugu wa kweli baina yake na Tanzania.
Amesema
kuwa Serikali ya Kenya kupita vya vyombo ulinzi na usalama vimefanya
kazi nzuri inayodhirisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na
Kenya, na ameeleza kuwa kama kusingekuwepo na ushirikiano
huo dhahabu na pesa hizo zilizokamatwa kwenye uwanja wa Jommo
Kenyatta nchini humo visingelejeshwa Tanzania.
“Tunaipongeza Serikali
ya Kenya kupitia vyombo vya vyake vya ulinzi vilivyofanya kazi nzuri ya
kukamata dhahabu kilo 35.34 iliyokuwa imeshavuka kwenye mipaka yetu,
na tuwapongeze pia kwa kutunza pesa yetu ambayo ilibiwa Tanzania
kwenye Benki ya NMB mwaka 2004, kwa kweli huu ni uaminifu mkubwa” amesema Rais
Magufuli
Licha ya
kuipongeza vyombo vya ulinzi vya Kenya Rais Magufuli ameshangazwa na
ukimya kutaka vyombo vya ulinzi vya Tanzania na hivyo kuvitaka
kujitafakari kwa namna dhahabu hiyo ilivyoweza kukamatiwa Kenya na
Sio Kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ambapo watuhumiwa walitumia
ndege ya ‘Precision Air’ kusafirisha mzigo huo.
“Vyombo
vyetu vya ulinzi vipo hapa lazima niviseme, dhahabu iliwezaje kufika Kenya
tukashindwa kuwakamata watumiwa wakiwa bado kwenye uwanja wa Mwanza?, hapa
lazima vyombo vyetu mjitafakari japo mnafanya kazi kubwa lakini ikiwezekana
mkajifunze kwa wenzenu wawape mbinu walizozitumia katika hili” amesema Rais
Magufuli.
Katika hafla
hiyo, Rais Magufuli pia alimpigia simu ya moja kwa moja Rais Uhuru
Kenyatta na kutoa shukrani zake na kumdhibitishia kuwa amepokea mzigo huo na
kumpongeza kwa ushirikiano wa Serikali yake kwa Watanzania, ambapo Rais
Kenyatta akimuhakikishia Rais Magufuli ushirikiano wa kudumu ambao utachochea
zaidi maendeleo kama walivyohaidi na kupewa mamlaka na wananchi.
Naye mjumbe
maalumu aliyemwakilisha Rais Kenyatta, Monica Juma ambaye ni Waziri wa Mambo ya
Nje wa Serikali ya Kenya amesema Serikali ya Kenya itaendeleza ushirikiano wake
na Tanzania katika masuala ya ulinzi na usalama kwa kuwa ushirikiano
huo utasaidia kukuza uchumi wa pande zote mbili.
Na kwa upande
wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba
Kabudi amesema Kenya na Tanzania ni ndugu tokea ezi na enzi, hivyo Serikali
Tanzania itahakikisha kuwa inaendelea kushirikiana na Kenya ili kufanya
ushirikiano huo unaleta manufaa kwa wananchi wa nchi hizo.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment