- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka wizara ya Maliasili
na Utalii kutenganisha eneo la uwindaji Selou (Hunting block) kwa kutengeneza
Hifadhi ya Taifa ambayo itaitwa Hifadhi ya taifa ya Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa kufua
umeme wa mto Rufiji mkoani Pwani utakaozalisha megawatt 2,115, Rais Magufuli
amesema kuwa eneo la uwindaji la Selou ni eneo ambalo limezunguka mradi huo
mkubwa wa umeme na lina urefu wa
kilomita za mraba elfu 57.
“Eneo la Selou ni eneo kubwa ambalo linachukua takribani
kilomita 50, hivyo ni lazima Wizara itenge eneo ambalo litatengenezwa na kuwa
Hifadhi kuweza kukidhi mahitaji ya utalii na kukisaidia kizazi kijacho
kuendelea kuenzi mambo ambayo ameyafanya baba wa Taifa,” amesema Rais Magufuli.
Amesema maeneo ya uwindaji wa wanyama yanafikia 47 katika
mbuga ya wanayama Selou hivyo Wizara ya Maliasili lazima itenge eneo la hifadhi
na la uwindaji, ili kuimarisha utalii na kuvutia watalii wengi katika mbuga
hiyo
Rais Magufuli alisisitiza kuwepo kwa utaratibu kwa Wizara ya
Maliasili na Utalii kuangalia maeneno ambayo yanavitalu wa uwindaji ili
kuhakikisha kuwa Serikali inafaidika na maeneno hayo, pia aliagiza barabara ya
kutoka Fuga kilomita 60 kwenda mahari ambapo mradi unajengwa ianze kutengenezwa
kwa rami ili kufungua sekta ya utalii katika Mbuga ya wanayama Selous.
Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa mradi wa kufua umeme wa
mto Rufiji ni mradi ambao unaweza kudumu kwa muda wa miaka 60 ambapo utasaidia
kuzalisha umeme wa kutosha na kusaidia Tanzania kuweza kutekeleza malengo ya
milenia ya maendeleo endelevu.
Amesema mradi wa mto Rufiji utasaidia kuchochea maendeleo
katika sekta ya viwanda ambapo wewekezaji wataweza kupata umeme wa uhakika na
kwa bei nafuu na wenye kuaminika ili kuweza kuzarisha bidhaa zenye ubora.
“Mradi huu wa umeme wa mto Rufiji unaweza kudumu kwa muda wa
miaka 60 na kusaidia watanzania kupata umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu
ambao utasaidia wawekezaji kupata huduma ya umeme kwa uhakika bila mgao ili
kuweza kuzarisha bidhaa zenye ubora na kuweza ushindano kwenye masoko
mbalimbali ya kimataifa,” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alisisitiza kuwa katika utekelezaji wa mradi
huo, mkandarasi anatakiwa kutumia wafanyakazi walioko karibu kwa kazi ambazo
siyo za kitaalamu, akasisitiza ajira zitolewe kwa wenyeji wa maeneo ya mradi
kwa mikoa ya Morogoro na Pwani, na amewataka wananchi kuchangamkia fursa kwa
miezi hiyo 36 ya ujenzi.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema
kuwa Ndoto ya Rais Magufuli ya kuenzi mambo makubwa ya Baba wa Taifa,
Mwl.Julias Nyerere ikiwemo utekelezaji wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme katika
maporomoko ya maji ya mto Rufiji.
“Mhe. Rais, ndoto yako leo imeanza kupata mafanikio, ndoto
yako ni kupeleka umeme hadi kule kijijini kwa wananchi wa kawaida na umetoa
agizo kuwa kila nyumba ya mtanzania iwe ya bati, nyasi au tembe lazima iwake
umeme, kwa hiyo umeme huu ambao ujenzi wake umezinduliwa leo ni kukamilisha
azma yako bila kujali maisha ya watanzania”, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu alisema kuwa kampuni zinazojenga mradi huo
mkubwa wa kufua umeme Tanzania, Els weldey na Arab Contructors, zinafanya kazi
nzuri kwa hiyo zitatekeleza mradi huo kwa weledi mkubwa, kama zinavyofanya kule
Misri.
Naye Waziri wa Nishati amesema mradi huo unabainisha mambo
mawili ya kumuenzi Rais wa kwanza Tanzania, hayati Julius Nyerere, ambayo Rais
Magufuli anatekeleza likiwemo kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda Dododma,
ambayo tayari yanatekelezwa, likiwemo la ujenzi wa Bwawa la Rufiji.
“Naomba niwakumbushe watanzania Mhe. Rais ametengeneza mambo
makubwa mawili ya ndoto ya baba wa Taifa ikiwemo kuhamisha makao makuu ya nchi
kwenda Dododma na utekelezaji wa mradi
mahususi wa bwawa la kufua umeme, mradi mkubwa
wa kwanza Tanzania, Afrika Mashariki na wa nne barani Afrika, huku
ukiingia kwenye mabwawa 70 makubwa duniani yakuzarisha umeme,” Waziri Kalemani.
Aidha Waziri Kalemani amesema kuwa mradi huu utekelezaji
wake utachukua miezi 42 ambapo hadi sasa miezi sita imeshapita na kubaki miezi
36 kukamilisha ujenzi wa mradi huo ambao unategemewa kukamilika Juni 13, 2022.
Waziri Kalemani aliongeza kuwa katika ujenzi wa mradi huo
kazi kubwa ya mkandarasi ni pamoja na ujenzi wa bwawa kubwa litakaloweza
kuhifadhi maji ya mita za ujazo billioni 33.2, ujenzi wa Power house
itakayokuwa na mashine tisa zenye kuzalisha megawati 235 kwa kila mashine na
kazi ya mwisho ni kujenga substation yenye kilovolt 400, ambapo ni umeme mkubwa
utakaotumika kwenye uchumi wa viwanda.
Umeme huo utasafirishwa kutoka Rufiji kwenda Chalinze umbali
wa kilomita 127 kwa dola za kimarekani 188 Chalinze mpaka Dar es Salaam na
Dodoma na ndio umeme utakao tumika kuendesha Treni ya kisasa (SGR), lengo la
Serikali ni kufikisha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025 kwahiyo mradi huu
mkubwa ni kichocheo kikubwa sana kuelekea uzarishaji wa hizo megawati.
Kwa upande wake Waziri wa nishati na umeme kutoka Misri Dkt.
Mohamed Shaker amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unaimarisha mahusiano ya
Tanzania na Misri katika sekta mbalimbali, ikiwemo ya nishati.
“Ujenzi wa mradi huu mkubwa ni moja ya hatua kubwa katika
mahusiano ya nchi mbili ambayo itahamasisha zaidi utekelezaji wa miradi mingine
ya undugu kati ya Tanzania na Misri, hususani kwenye nyanja ya umeme, nipende
kusisistiza kwamba mradi huu wa umeme Rufiji unaungwa mkono na Rais wa Misri,
Abdel Fattah El-Sisi” Waziri Shaker.
Nchi ya Misri itaendelea kushirikiana na Tanzania katika
utoaji wa mafunzo ya teknolojia ya kuzalisha umeme, kwani ina vituo 22 vya
kutolea mafunzo hayo na imetoa nafasi 50 kwa wataalamu kutoka Tanzania kwenda
kujifunza masuala ya ufuaji na uzalishaji umeme.
Comments
Post a Comment