- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Constantine Kanyasu akizungmza
kwenye mkutano kati ya wananchi na Mbunge kuhusu ahadi mbalimbali alizozitekeleza ikiwemo suala la utoaji mikopo wa
shilingi bilioni 1.6 kwa vikundi
mbalimbali wakiwemo vijana, wanawake na walemavu kwa lengo la kupunguza umasikini katika jamii
kwenye mkutano uliofanyika katika kata
ya Ihanamiro wilaya ya Geita mkoani Geita.
Mbunge wa
Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine
Kanyasu amesema Halmashauri ya mji wa Geita hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu
tayari imeshatoa mkopo wa Shilingi
bilioni 1.6 kwa ajili ya wakinamama, vijana na walemavu kwa lengo la kutimiza adhima ya Serikali ya awamu ya tano chini ya
uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.
Amesema
lengo la kutoa mkopo huo ni kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na kuweza
kuinua kipato cha wananchi kwa kunufaika na miradi mbalimbali na hatimae kuweza
kujikwamua kiuchumi.
Hayo
ameyasema kwenye mkutano wakati akizungumza na wananchi wake kuhusu ahadi
mbalimbali alizozitekeleza ikiwemo ya kutoa mkopo wa shilingi bilioni 1.6 kwa
vikundi mbalimbali kwa lengo la kupunguza umasikini katika jamii katika mkutano
huo uliofanyika katika kata ya Ihanamiro wilaya ya Geita mkoani Geita.
Mhe.Kanyasu
amewaeleza wananchi hao kuwa kutokana na uhusiano mzuri uliopo miongoni mwa
madiwani katika Halmashauri hiyo wameweza kutoa mkopo huo. Hata hivyo amesema
kuwa mikopo hiyo itasaidia katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo
vitasaidia kutengeneza ajira na kukuza uchumi
Akizungumza
katika mkutano huo,Mhe.Kanyasu amesema anajisika fahali ya kutoa mikopo hiyo kwa vikundi ikiwa ni moja
ahadi alizozitimiza za kuhakikisha mwananchi wake wanajihusisha kwenye shughuli
za kiuchumi ili kupunguza umasikini kuanzia ngazi ya familia hadi taifa
Amesema
kuwa kutokana na changamoto zilizoko
katika taasisi za fedha, ambazo hutoa mikopo kwa riba kubwa na kuhitaji
dhamana ya nyumba na ardhi jambo ambalo linawakwamisha wakopaji hivyo serikali
imeamua kutoa mikopo ya masharti nafuu.
Aidha
amesema mikopo hiyo itawasaidia makundi
hayo kuweza kuongeza mitaji na kutoa
ajira ndani ya jamii.
Aidha,
Mhe, Kanyasu amesema katika awamu ya pili ya utoaji mkopo wataongeza viwango vya mikopo kwenye vikundi
ambapo kila kikundi kitakuwa na uwezo wa kukopeshwa hadi kufikia shilingi
milioni 20 tofauti na ilivyokuwa awali
Kwa upande
wake, Diwani wa kata ya Ihanamiro, Mhe.
Joseph Lugaira amemueleza Mbunge huyo kuwa katika kata hiyo jumla ya vikundi 19
vimenufaika na mkopo huo kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi.
Amesema
vikundi hivyo vimekuwa vikifanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo
biashara pamoja na kilimo ambapo anaamini wataweza kupata faida pamoja na
kurejesha mkopo huo na kukopa tena.
Naye
Diwani wa viti maalum, Mhe. Suzana Mashala
amewahimiza wanawake wasiogope kukopa kwani hawawezi kujiendeleza
kiuchumi pasipo kukopa.
Vile vile,
Diwani huyo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanawake waliokopa wajitahidi
kurejesha mikopo hiyo mapema ili mikopo hiyo iweze kuwasaidia watu wengine
lengo likiwa ni kuondokana na umasikini.
Kwa upande
wake, Emalio Nyangabo ambaye ni kiongozi wa Kikundi cha Tuinuane, amesema walipokea mkopo ambao umewasaidia
kuinuka kiuchumi, na kuwawezesha kufanya
shughuli za uzalishaji mali na kuachana na kujihususha na vitendo visivyofaa
katika jamii
Naye,
Godson Maduka ambaye ni miongoni mwa vijana walionufaika wa mkopo huo amesema
mkopo huo umewasaidia vijana wengi kujiepusha kujiingiza kwenye utumiaji wa
madawa ya kulevya na unywaji wa pombe kupita kiasi.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Geita,
Mhe.Mohamed Ali( wa pili kulia) pamoja na Diwani wa kata ya Ihanamiro, Joseph
Lugaila wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kabla Mhe. Kanyasu kuanza kuzungumza
na wananchi wake katika kata ya Ihanamiro.
Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria mkuatano wa
Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine
Kanyasu wakimsikiliza wakatik akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu
ahadi alizozitekeleza kwa wananchi wake likiwemo suala la mikopo kwa wanawake,
vijana na walemavu.
Baadhi ya Madiwani wa viti maalum walioshirki kwenye
mkutano wa Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine Kanyasu wakimsikiliza wakati
akizungumza na wananchi wake katika kata ya Ihanamiro.
Baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye mkutano wa
Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine Kanyasu wakimsikiliza Mbunge wao
wakati alipokuwa akizungyumza nao katika kata ya Ihanamiro.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita, Mohamed Ali, akizungumza na wananchi wa kata ya Ihanamiro kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri
wa Maliasili na utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini kabla ya kuzungumza
na wananchi wa kata hiyo.
Comments
Post a Comment