- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Doroth Mwaluko akifungua
mafunzo kwa watumishi wa Ofisi hiyo wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma
hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma.
Na
Mwandishi Wetu
Watumishi
wanaotarajia kustaafu wameaswa kuzingatia mabadiliko ya maisha kutoka katika
utumishi wa umma kwenda katika mfumo wa maisha ya kawaida na kujiepusha kufanya miradi ambayo
hawana ujuzi wa kutosha kuihusu.
Akizungumza katika mafunzo kwa yakuwajengea
uwezo watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni ili
wawe na mbinu za kuendana na mazingira hayo, Katibu Mkuuu wa Ofisi hiyo
anayeshughulikia (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Doroth Mwaluko amesem kuwa
Ofisi hiyo inatambua umuhimu wa wastaafu na faida za kujiandaa kustaafu.
“ Kuna umuhimu mkubwa wa kutambua kuwa suala la kustaafu
ni la kila mmoa wetu na ni muhimu kujiandaa vyema na maisha mapya ambayo
kimsingi yatakuwa tofauti na haya ya utumishi wa umma mliyo nayo kwa sasa” Alisisitiza Mwaluko
Akifafanua amesema kuwa kila mtumishi wa umma
lazima atambue kuwa ni mstaafu matarajiwa hivyo kujiandaa kwake ni jambo muhimu.
Kwa upande wake Muwezeshaji Kutoka Chuo cha
Utumishi wa Umma Magogoni Jijini Dar es Salaam Bw. Peter Seme amesema kuwa
watumishi hao wanaotarajia kustaafu watajifunza mambo mengi yakuwawzesha
kuendelea na maisha yao kama kawaidia hata baada ya kustaafu.
Alitaja baadhi ya mada kuwa ni pamoja na utayari
wa kupokea mabadiliko baada ya kustaafu, Stadi za kuongeza kipato, Mtindo wa
maisha bora baada ya kustaafu, Namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza
kujitokeza baada ya kustaafu.
Kwa upande wake mmoja wa watumishi hao Bw. Esamo Sawaki amesema kuwa wanaipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa
mafunzo hayo kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi hiyo ili waweze
kukabiliana na changamaoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kupata
uzoefu kutoka kwa wastaafu wengine ambao tayari wana uzoefu katika kukabiliana
na changamoto za kustaafu na hata kuelewa kazi ambazo ni za uzalishaji
wanazoweza kuzifanya kama wastaafu ili kuwaletea tija.
“Tutapata maarifa sahihi ya namna ya kutumia
kiinua mgongo tutakachopewa baada ya kustaafu kutoka katika utumishi wa umma”
Alisisitiza Sawaki
Mafunzo yakuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni yanafanyika Jijini Dodoma kwa
siku tano yakiwashirikisha watumishi hao kutoka kada mbalimbali.
Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Doroth Mwaluko akisisitiza
umuhimu wa mafunzo kwa watumishi wa
Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo
June 17, 2019 Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bi Mazoea Mwera akizungumza
wakati wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi hiyo wanaotarajiwa kustaafu utumishi
wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa
Fedha wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA)
Bi Monica Robert akizungumza wakati wa
mafunzo hayo kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa kustaafu
utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma.
Muwezeshaji
kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma
Magogoni Bw. Peter Seme akizungumza katika
mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa kustaafu
utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Doroth Mwaluko (Katikati walioketi)
akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa
kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma mara
baada ya kufungua mafunzo hayo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kustaafu.
(Picha na Frank
Mvungi- MAELEZO)
Comments
Post a Comment