- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Serikali
imesema mabadiliko kwenye sekta ya sheria nchini hususani Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu yameanza kuleta tija baada ya kuongeza ufanisi na kuokoa fedha ambazo hapo
awali zilikuwa zikitumika kuwalipa mawakili binafsi.
Akijibu
swali la Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea ambae alitaka kujua kiasi cha
fedha ambacho serikali imeokoa tangu maboresho kwenye sekta hiyo yaanze
kutekelezwa, ambapo pamoja na mambo mengine yalianzisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa
Serikali ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia, kuendesha na kuratibu mashauri
yote ya madai kwa niaba ya Serikali nchini.
Kwenye
majibu yake Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga alimueleza mbunge
hyo kuwa kwenye Mwaka wa Fedha 2018/19 pekee Serikali imeweza kuokoa zadi ya
shilingi bilioni tisa (9,018,957,011), ambazo kama sio maboresho kwenye sekta
hiyo zingetumika kulipa makampuni binafsi ya uwakili.
Aidha,
Dkt. Mahiga aliendelea kulieleza Bunge kuwa Serikali itaendelea kutumia
Mawakili binafsi kwa kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale
itakapothibitika kuwa ni lazima kufanya hivyo. Alitoa mfano wa vigezo vinavyotumika
kutumia mawakili binafsi ni shauri kufunguliwa kwenye mahakama ambazo sio za
kimataifa na sheria za nchi husika haziruhusu uwakilishi wa mwanasheria kutoka
nje ya nchi hiyo.
Kuhakikisha
maslahi ya taifa yanalindwa Dkt. Mahiga ameliambia bunge kuwa uendeshaji wa
mashauri hayo utendelea kuishirikisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye
kila hatua ya mwenendo wake tofauti na hapo awali.
Kuhusu
baadhi ya mashirika ya umma kuendelea kutumia mawakili binafsi, Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi amelieleza Bunge kuwa mashirika hayo
ni yale ambayo mashauri yake yalianza kabla ya maboresho kwenye sekta hiyo hayajaanza
kutekelezwa na uendeshaji wa mashauri utatekelezwa kwa kushirikiana na Wakili
Mkuu wa Serikali.
Comments
Post a Comment