- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Kamishna
wa Uhifadhi wa TANAPA Dk. Allan Kijazi akishuhudia uvishwaji wa cheo kwa Naibu
Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo wa TANAPA William Mwakilema uliofanywa
na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania
TANAPA, Jenerali Mstaafu George Waitara.
Baadhi ya
viongozi wapya wa jeshi-usu la Uhifadhi wakila kiapo cha utii katika hafla ya
kutunuku vyeo vipya kwa watendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania. Hafla
hiyo imefanyika katika Kituo cha Mafunzo ya jeshi-usu, Mlele mkoani Katavi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA Jenerali
Mstaafu George Marwa Waitara akimvisha cheo cha Kamishna Mwandamizi Kanda ya Kusini
Dk Christopher Timbuka
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania Jenerali
Mstaafu George Marwa Waitara akimvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mawasilino TANAPA Pascal Shelutete katika hafla ya uvishaji vyeo kwa
Maafisa wa TANAPA.
Kamishna Msaidizi
Huduma za Shirika Kanda ya Kusini Rukia Mkakile akiwa kwenye
ukakamavu huku akipiga saluti kama heshima baada ya kuvishwa cheo hicho na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania
TANAPA Jenerali Mstaafu George Waitara ambaye hayupo pichani
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA Generali Mstaafu George Marwa Waitara
akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi usu.
Wahitimu
wa mafunzo ya jeshi-usu wakipita kwa mwendo wa haraka katika gwaride
la utoaji wa vyeti kwa wafanyakazi wa TANAPA, Gwaride hilo lilikaguliwa
na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu ,George Waitara .
Baadhi ya
watendaji wapya wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi
za Taifa Tanzania TANAPA Jenerali Mstaafu Geogre Marwa Waitara
katika hafla ya kutunuku vyeo vipya kwa watendaji wa Shirika la Hifadhi
za Taifa Tanzania TANAPA
Picha ya
pamoja ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA na Makamishna
Wandamizi mara baada ya kuvikwa vyeo hivyo wakati wa halfa hiyo iliyofanyika katika
kituo cha mafunzo ya jeshi-usu Mlele mkoani Katavi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
Mweyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa ,Jenerali (Mstaafu) George Waitara amezindua mfumo mpya wa utendaji kazi ndani ya Hifadhi za Taifa unaopeleka madaraka zaidi katika ngazi ya Kanda nne kuu zilizoundwa ili kuboresha utendaji kazi unaoendana na mfumo mpya wa jeshi -usu.
Uzinduzi huo ulienda sambamba na zoezi la utoaji vyeo vipya vilivyoidhinishwa na bodi ya wadhamini kwa viongozi wa shirika ambao ni Naibu Kamishna wa Uhifadhi wawili, Makamishna wa Uhifadhi wa kanda wanne, Makamishna Wasaidizi Waandamizi 14, Makamishna wasaidizi 22 pamoja na Maafisa Wakuu na Waandamizi saba.
Muundo mpya unahusisha Kanda ya Kaskazini yenye Hifadhi za Arusha, Tarangire, Ziwa Manyara, Kilimanjaro na Mkomazi ,Kanda ya mashariki inayojumuisha Hifadhi za Saadan, Mikumi na Udzungwa, Hifadhi za Ruaha na Kitulo na Katavi zitakuwa chini ya usimamizi wa kanda ya Kusini.
Kanda ya Magharibi itasimamia Hifadhi za Taifa za Gombe, Mahale, Kisiwa cha Saanane, Kisiwa cha Rubondo, Serengeti pamoja na Hifadhi mpya za Burigi, Kimisi, Biharamulo, Ibanda na Rumanyika.
Hafla hiyo pia imeendana na zoezi la kuwatunuku vyeti wahitimu 217 wa mafunzo yaliyochukua miezi sita kwa awamu mbili yakihusisha Maafisa wa Uhifadhi pamoja na waajiriwa wapya.
Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwawezesha wahitimu kufanya kazi kwa mfumo wa kijeshi -usu katika kuboresha utendaji kazi na majukumu ya usimamizi thabiti wa maliasili zilizopo hifadhini kwa kuwajengea wahitimu uwezo wa kimwili ,kisaikolojia,kimaadili na uzalendo.
Comments
Post a Comment