- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
IDADI YA MADAKTARI NA WATOA HUDUMA ZA AFYA WALIOPATIWA MAFUNZO NA WCF KUHUSU NAMNA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI ZITOKANAZO NA KAZI YAFIKIA 856
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Baadhi
ya madaktari na watoa huduma za afya wakionesha stika watakazobandika
kwenye ofisi zao, mara baada ya kushiriki mafunzo ya siku tano ya namna
ya kufanya tahmni ya ugonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
yamefungwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mei 10, 2019.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
MFUKO wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) tayari umeweza kumetoa mafunzo kwa madaktari na watoa huduma
za afya 856 Tanzania Bara kuhusu namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali
zitokanazo na kazi
Akizungumza muda mfupi
kabla ya kumkaribisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kufunga mafunzo ya wiki
moja kuhusu namna ya kufanya tathmini hiyo mjini Morogoro Mei 10, 2019,
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omary
alisema idadi hiyo ni kuanzia mwaka 2015 tangu Mfuko huo uanze kutekeelza
majukumu yake hadi kufikia Mei 10, 2019.
Alisema washiriki
waliohudhuria mafunzo ya Morogoro wanatoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar
es Salaam na Morogoro na licha ya kufundishwa namna ya kufanya tathmini washiriki
pia walifundishwa shughuli za Mfuko ili wao nao wawe mabalozi pindi
watakaporejea kwenye vituo vyao vya kazi.
Akifunga mafunzo hayo,
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Frank Jacob. Aliushukuru Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kutoa elimu hiyo kwani itasaidia sana kuongeza uwezo
wa madaktari katika kutekeleza jukumu hilo kubwa la kufanya tathmini kwa
mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi.
“Nahakika katika
kipindi hiki mlichokuwepo hapa mtakuwa mmejifunza mambo mengi mapya na kuwapa
ujuzi ambao huenda hamkuwa nao wakati mnakuja hapa.” Alsiema Dkt. Jacob.
“Mimi
toka nimeanza kufanya kazi ya udaktari nina miaka 15 lakini ukiniuliza namna
gani unaweza kufanya tathmini kwa mtu aliyepata ajali maeneo ya kazi bado
nilikuwa Napata shida, nilikuwa najikanyaga kanyaga sikuwa na uelewa kuhusiana
na tathmini ya watu waliopata ulemavu katika maeneo ya kazi.”Alisema
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akimkabidhi stika, Bi. Rosemary K. Mbaule kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt.Abdulsalaam Omary, akitoa hotuba ya utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga mafunzo hayo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Frank Jacob, akitoa hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo. |
Dkt. Frank Jacob, (wa pili kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF), Dkt. Ali Mtulia, (wa tatu kushoto), Dkt. Robert Mhina, (wa kwanza kushoto), kiongozi wa jopo la watoa mada,na Dkt. Hussein Mwanga Mhadhiri MUHAS.
Dkt. Pascal Magessa kutoka WCF, akitoa mada juu ya namna ya ulipaji Fidia.
Dkt. Pascal Magessa kutoka WCF, akitoa mada juu ya namna ya ulipaji Fidia. |
Dkt. Pascal Magessa kutoka WCF, akitoa mada juu ya namna ya ulipaji Fidia. |
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki kutoka Dar es Salaam |
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na watoa mada.
Comments
Post a Comment