- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mshauri wa afya ya watoto wachanga Dk. Samira Aboubakar
akijadiliana na baadhi ya washiri wa mafunzo ya watoto wachanga katika Hoteli
ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja. Picha zote na Makame Mshenga.
Na Ramadhani Ali,
Maelezo - Zanzibar
MKURUGENZI Kinga na Elimu ya
Afya Zanzibar Dk. Fadhil Mohd Abdalla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inaendelea kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya watoto wachanga chini ya mwezi
mmoja vinavyotokana na maambukizi.
Aliitaja mikakati hiyo kuwa ni
pamoja na kuhakikisha huduma za maradhi ya maambukizi yanayowasumbua watoto
ndani ya wiki ya kwanza tokea kuzaliwa zinatolewa katika vituo vyote vya
afya badala Hospitali kuu pekee.
Dk. Fadhil alitoa kauli hiyo
alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya madaktari wakufunzi kutoka nchi za
Afrika Mashariki na Kati katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi.
Alisema Zanzibar imepiga hatua
kubwa katika kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa mwaka mmoja hadi mitatu
lakini vifo vya watoto wachanga wa siku saba za mwanzo tokea kuzaliwa bado
imekuwa ni changamoto.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya
Afya alisema Wizara itaendelea kufundisha Madaktari wa vituo vya ya afya msingi
ili kuhakikisha kila kituo kinaweza kutoa tiba ya maambukizi.
“Lengo ni kuhakikisha dawa za
maambukizi zilizokuwa zikitolewa Hospitali kuu sasa zinasambazwa katika vituo
vya afya ili kupunguza vifo vya watoto wachanga” alisisitiza Dk. Fadhil.
Mwakilishi wa Shirika la Afya
Ulimwenguni (WHO) Ofisi ya Brazzaville Congo, ambae ni mtaalamu wa afya ya
watoto wachanga Dk. Assumpta Muriizhi, alisema akinamama wanapitia kipindi
kigumu katika kipindi cha miaka miwili baada ya kujifungua kutokana na
kupambana na afya ya mtoto ambae hawezi kujieleza.
Alisema wapo baadhi ya wazazi
hawaoni umuhimu wa kuwapeleka watoto wao Hospitali wanapopata maambukizi jambo
linapelekea kuathirika zaidi na hatimae kupoteza maisha.
Aliwashauri akinamama
wanapogundua watoto wao wachanga wanasumbuliwa na maradhi kuwawahisha mapema
vituo vya afya vya karibu kupata huduma ya awali kabla ya kuwapelekwe Hospitali
kuu iwapo matatizo yataongezeka.
Alisema hakuna umuhimu mkubwa
kwa watoto wachanga kuwaanzisha huduma za afya katika Hospitali kuu hasa kwa
Zanzibar ambapo vituo vya afya vinapatikana kila sehemu.
Mkutano huo unahudhuriwa na
Madaktari Wataalamu wa watoto wachanga kutoka Zambia, Zimbabwe,
Msumbiji, Kenya, Uganda, Tanzani Bara, Zanzibar na Maafisa
Wawakilishi wa Mashirika ya
Kimataifa ya WHO na UNICEF.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Ofisi ya
Brazzaville Congo Dk. Assumpta Muriizhi akizungumza na washiriki wa mafunzo ya
madaktari wa watoto katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Fadhil
Mohamed Abdalla akifungua Mafunzo ya siku tano ya madaktari wa watoto wachanga
kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi
Mjini Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya madaktari wa watoto
wachanga kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati wakimskiliza Mkurugenzi Kinga
na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Fadhil Mohd Abdalla (hayupo pichani) alipokuwa
akifungua mafunzo hayo.
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo ya siku tano ya
madaktari wakufunzi wa watotot wachanga kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati
na mgeni rasmi.
Comments
Post a Comment