- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula akisalimiana na Msajili wa Bodi ya Usajili Wataalamu Mipango Miji Hellen Mtutwa alipokwenda kufunga Mkutano wa tano wa Bodi jana jijini Dodoma, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Welbert Kombe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula akifunga mkutano wa tano wa Bodi ya Usajili Wataalamu wa Mipango Miji jijini Dodoma Jana.
Sehemu wa washiriki wa Mkutano wa tano wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji uliofanyika jijini Dodoma. (Picha zote na Hassan Mabuye wa Wizara ya Ardhi)
Na Munir Shemweta,
Dodoma
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk
Angeline Mbaula amewataka wataalamu wa mipango miji kuwa na mipango
endelevu na kabambe katika miji na
halmashauri zote nchini ili kuwa na miji iliyopangika na kuepuka ubomoaji
nyumba za wananchi unaosababishwa na uelewa mdogo wa sheria na taratibu za
mipango miji..
Aliwataka wataalamu wa mipango miji kuwajibika ipasavyo
katika kutekeleza majukumu yao kuepesha wananchi kuvunja sheria unaosababishwa
na wataalamu kutowaeleza ambapo alisema si kila mwananchi anayevunja sheria za
ujenzi mjini anafanya makusudi bali wengine hawajui sheria na taratibu na
kuhitaji kuelezwa.
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa tano wa Bodi ya
Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji
jijini Dodoma jana, Dk Mabula alesema maeneo mengi ya miji wataalamu
wanahangaika na kazi ya kurasimisha jambo ambalo siyo suluhisho la upangaji
miji bali ni kujaribu kuweka viraka katika vazi lililochakavu.
Akigeukia suala la kuwepo maeneo mengi yasiyopangwa, kupimwa
na kumilikishwa Dk. Mabula alisema eneo hilo linaibua changamoto mbalimbali kwa
jamii ikiwemo ongezeko la makazi holela maeneo
ya mijini, kukua kwa miji isiyo na mpangilio mzuri pamoja na kukithiri kwa
migogoro ya ardhi nchini na kuwashauri wataalamu hao wa Mipango mijini nchini kuwafuata
wananchi waliko kwa ajili ya kutatua kero zao.
Alizitaka halmashauri ambazo muda wa mipango yake kabambe imeisha
kuhakikisha zinahuisha mipango hiyo ili
kuwa endelevu kwa minajili ya kuweka miji salama na ikiwa imeandaliwa miundo
mbinu muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya miji na taifa kwa ujumla.
Aidha, Dk. Mabula ametaka maeneo ambayo reli ya SGR inapita
ni vyema halmashauri za maeneo husika kuanza kufanya upangaji mapema ili reli itakapoanza
maeneo yote yawe yamepangwa, yamepimwa na yamemilikishwa na uendelezaji
umefanyika ili kuinua uchumi kwa maeneo husika na kutosubiri wajanja wakaanza
kuvamia.
Katika maazimio yake yaliyosomwa na Msajili wa Bodi ya Usajili
wa Wataalamu Mipango Miji Hellen Mtutwa, Washiriki walikubaliana Chuo Kikuu cha
Ardhi kwa kushirikiana na Bodi ya Usajili Wataalamu Mipango Miji kuandaa
muongozo utakaowawezesha Watendaji wa Kata na Vijiji kuwa wasimamizi wa mipango miji kwenye maeneo yao ili kuepuka ujenzi
holela na miji isiyopangwa.
Aidha, Washiriki walikubaliana urasimishaji wa makazi
ufanayike katika maeneo yote ya nchi na siyo baadhi ya maeneo na wataalamu
mipango miji kuhakikisha wanaandaa andiko la mradi kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya upangaji miji badala ya kusubiri serikali pekee.
Mkutano huo wa Bodi ya Usajili Wataalamu Mipango Miji
uliokuwa ukijadili matatizo na changamoto zinazowakabili Wataalamu wa taaluma
za Mipango Miji katika shughuli zao na
kuweka mikakati ya kukabiliana nazo na
kushirikisha wataalamu 260 kutoka Serikali na Sekta Binafsi pamoja na Makampuni
yanayojishughulisha na mipango miji.
Comments
Post a Comment