- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
SERIKALI YA TANZANIA YAANZA MAZUNGUMZO NA UJERUMANI YA MGAO WA MAPATO YATOKANAYO NA MJUSI MKUBWA ‘DINOSAUR’ KUPITIA WATALII
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Baadhi ya mabaki ya Mjusi mkubwa mwenye urefu wa mita
13.7 kwenda juu aliyegunduliwa miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru
mkoani Lindi aliyepo katika makumbusho nchini Ujerumani ambao kwa sasa Serikali
ya Tanzania imeanza mazungumzo kuona jinsi gani itaanza kupata gawio lake
kupitia watalii.
Serikali ya Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Japhet Hasunga imesema ipo kwenye
hatua za awali za mazungumzo na Serikali ya Ujerumani kuona jinsi
itakavyofaidika na mapato yatokanayo na utalii
kupitia mabaki ya Mjusi mkubwa ‘’Dinosaurs ambaye ni kivutio cha kikubwa
cha utalii katika jumba la Makumbusho nchini Ujerumani
Mjusi huyo kwa jina la kitaalamu anaitwa Dinosaur ambapo mabaki yake yalivumbuliwa miaka
100 iliyopita katika eneo la Tendaguru
mkoani Lindi, yalikusanywa na kupelekwa nchini Ujerumani ambako wataalamu waliyaunda
na kisha kuyaweka kwenye Makumbusho hiyo.
Amesema lengo la mazungumzo hayo ni kutaka
kujua kiasi gani cha mapato
yanayokusanywa na namna gani wanavyoweza kugawana mapato hayo yatokanayo na watalii kupitia mjusi huyo
baina ya Serikali hizo mbili.
Amesema mwelekeo wa mazungumzo hayo
yaitapelekea Serikali ya Tanzania kufanya uamuzi wa kumrudisha mjusi huyo au kumuacha kule kule lakini akiwa
analiingizia pato taifa
Ameyabainisha hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa
habari kuhusiana na mIkakati ya Serikali
ya kuendeleza vivutio vya utalii kwa mikoa ya Kusini.
Hata hivyo, Mhe.Hasunga amesema uamuzi wa kumrudisha mjusi huyo nchini utakuwa mgumu kwa vile
sehemu kubwa ya mjusi huyo ameunganishwa unganishwa kwa kutumia vifaa maalumu.
Ameongeza kuwa kutokana na jinsi alivyounganishwa unganishwa na anakadiri
wa kuwa na urefu wa mita 13.7 kwenda juu
hivyo kumsafirisha itakuwa ngumu.
Katika hatau nyingine, Mhe Hasunga amesema hadi hivi sasa Serikali ya Ujerumani haijaweza kuweka bayana
kiasi cha mapato yanayokusanywa kupitia
Mjusi huyo licha ya kuwa Serikali hiyo
imekuwa ikifadhili miradi mingi ya uhifadhi nchini.
"Tunaamini kuwa pesa wanazofadhili miradi mingi ya Uhifadhi imekuwa
inatokana na makusany okupitia Mjusi huyo Mkubwa" amesema Hasunga
Hata hivyo,kuendelea kuwepo kwa masalia ya mjusi huyo katika Makumbusho
hiyo kuna manufaa makubwa kwa vile anatambuliwa kuwa ni wa kutoka
Tanzania,Hivyo ni Balozi wa Utalii na utafiti wa kisayansi anayeitangaza
Tanzania sehemu mbalimbali duniani.
Comments
Post a Comment