- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
MNEC MTEWELE ACHANGIA MIFUKO 50 YA SARUJI KWA AJILI YA UKARABATI WA MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI NJIA PANDA
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa (MNEC) Theresia Mtewele akimkabidhi cheti cha kuhitimu darasa la saba mwanafunzi wa shule ya msingi Njia Panda.
Mjumbewa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa (MNEC) Theresia Mtewele akicheza kwa furaha na wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya msingi Njia Panda.
Mjumkbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa (MNEC) Theresia Mtewele akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wahitimu wa darasa la saba wa shule ya msingi Njia panda.
NA FREDYE MGUNDA,IRINGA.
MJUMBE wa Halmashauri kuu ya chama
cha mapinduzi taifa (MNEC) Theresia Mtewele amechangia mifuko hamsini ya saruji
katika shule ya msingi Njia panda ambayo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya
madarasa kumi na nane pamoja na matundu thelathini na saba ya vyoo na
kusababisha kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi wa shule hiyo.
Akizungumza wakati wa mahafali ya
shule hiyo MNEC mtewele alisema kuwa hali ya miundombinu ya shule hiyo sio
rafiki kwa wnafunzi kupata elimu bora kama ambavyo serikali ya awamu ya tano
inakusudia
"Naiomba Serikali na wahisani
mbalimbali kuisaidia shule ya msingi hii kwa kuboresha miundombinu ya shule
hiyo ili kuwawekea mazingira bora ya kusoma wanafunzi ya kufanya vizuri kwenye
mitihani yao"alisema Mtewele
Mtewele alisema kuwa kwa mazingira
ambayo ameyaona ya miundombinu ya shule hiyo inahitajika nguvu ya ziada
kuhakikisha wanatatua changamoto hizo ambazo zimekuwa kikwazo cha kufanya
vizuri kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo
"Leo sijalidhishwa na hali hii
japo nimekuja kumuwakilisha mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi
Salim Asas nitaenda kumueleza ukweli jinsi ambavyo shule hii inahitaji msaada
mkubwa na wa haraka kwa kuokoa elimu ya wanafunzi Hawa" alisema Mtewele
Aidh MNEC Mtewele aliwaasa wahitimu
na wanafunzi wanaoendelea wasikubali kurubuniwa na watu wasiowafahamu kw kuwa
watawakatisha ndoto zao za baadaye zaidi wajikite katika masomo na kujiepusha
na magonjwa ambukizi.
Dunia ya sasa inaharibiwa sana na
watu ambai wanatumia vibaya mitandao ya kijamii hivyo ni lazima mjue jamii
ambayo mnaishi nayo inamalengo gani na je inafaida katika maisha yako ya baadae
ndio upate muelekeo na maamuzi sahihi kwa faida yako alisisitiza MNEC mtewele
Mtewele ameuahidi uongozi wa shule
kufuatilia utekelezaji wa ahadi kwa wabunge wote wa Mkoa wa Iringa ambao
walitoa ahadi zao katika shule hiyo miaka ya nyuma na ahadi hizo
hazikutekelezwa mpaka sasa
Katika risala iliyosomwa na Mwalimu
mkuu wa Federika Mahembepo shule hiyo alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na
upungufu wa zaidi ya madarasa 18 na matundu ya vyoo 37 ili kukidhi
mahitaji ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo.
Lakini mealimu mkuu wa shule hiyo
amewapongeza walimu na wazazi wa shule hiyo kwa kutambua kazi ngumu na nzito
wanayofanya kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu inayosatahili kama
ambavyo wanafunzi wengine wanapata Elimu bora na kuwaomba wazazi waendelee
kuiunga mkono serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa sababu imedhamilia
kushughulika na shida za watu.
Comments
Post a Comment