- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
KATIBU mkuu wa umoja wa vijana
wa chama cha mapinduzi (UVCCM) taifa kuwa mgeni rasmi katika uzindua albam ya nyimbo
za injili ya msanii James Mgego wa mkoani Iringa inayoitwa “Achani Mungu Aitwe Mungu” na
uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa HIGHLAND HALL uliopo mjini iringa
tarehe 30 /09 /2018.
Akizungumzia uzinduzi huo msanii
wa nyimbo za injili James Mgego alisema kuwa anatarajia kuzindua albam yenye
nyimbo tisa zilizotengenezwa katika studio za Nice zilizopo mkoani Iringa.
Mgego alisema kuwa mgeni rasmi
atakuwa katibu mkuu wa umoja wa vijana ndugu Raymond Mwangwala(MNEC) na
viongozi wengi wa serikali na wakisiasa kutoka mkoani Iringa na nje ya mkuoa wa
Iringa.
Katika uzinduzi huo kutakuwa na
kwaya mbalimbali ambazo zitatumbuiza kama vile TAC kwaya Anglicana, Nuru kwaya
Anglicana,TAG Mlandege,Mhimidini Mlandege,Kwaya ya vijana kanisa kuu,kwaya mkuu
kihesa,uinjilisti KKKT Ipogolo, uinjilisti KKKT PHM frelimo,kwaya ya vijana
kitwilu,RC Mshindo,ACT fellowship,Faith kwaya tumain, RC kichangani kihesa,Sayuni
Anglican Ipogolo na Elishadai Anglican Ilula.
Aidha Mgego alisema kuwa
kutakuwepo na waimbaji maalufu na mashuhuri wa nyimbo za injili ndani na nje ya
mkoa wa Iringa watakuwepo kama vile DR Tumaini Msowoya,Nesta Sanga,Ntimiza
Rwiza,Samson Kihombo,faraja kigula,Mwl Senje,mama masawe mwamvita,Petro
Chetenge,Raymond Mwalisu,Tukuswiga Ikoso na wengine wengi.
Mgego alisema kuwa
anawakabiribisha wananchi wote katika uzinduzi huo ambapo hakutakuwa na
kiingilio chochote kile.
Comments
Post a Comment