- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na WAMJW
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemwagiza mtaalamu bingwa wa uchunguzi kwenda mkoani Kagera kwa ajili ya kurejea uchunguzi wa chanzo cha kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius (13) wa shule ya Msingi Kibeta iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera na kuwahakikishia wanafamilia na wananchi kuwa uchunguzi utafanyika kwa ufanisi na haki itatendeka.
Ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumzia kuhusu kifo cha mwanafunzi huyo kinachosemekana kilisababishwa na mwalimu wake Respicius Patrick baada ya kumpiga kwa kumtuhumu
kumuibia pochi yake.
Waziri Ummy amesema kuwa kitendo hicho ni cha
ukatili kwani ni kinyume na Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 kifungu cha
13 (2) ambayo inasisitiza kutolewa kwa adhabu stahiki kwa mtoto kulingana na
umri, hali ya kimwili na kiakili.
Aidha, amelaani
vikali Vitendo vya Ukatili dhidi ya watoto vinvyoendelea kufanyika
katika jamii na kusema kuwa Serikali itahakikisha inawafuatilia na
kuwachukulia hatua watakaofanya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa wa kuwa suala hilo lipo mikononi
mwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi, anaamini pindi uchunguzi utakapokamilika
hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa.
Amesisitiza kuwa jamii na kila mtu
anaowajibu wakuhakikisha mtoto anaishi, kukua na kuendelezwa
katika mazingira salama na rafiki kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.
Comments
Post a Comment