- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
LONDON, ENGLAND
DIRISHA la uhamisho la klabu za Uingereza linafungwa leo Ijumaa lakini BBC michezo inaangazia makubaiano ambayo huenda yakakamilishwa barani
Ulaya.
Timu zilizopo nje ya Uingereza zinaweza kufanya makubaliano
ya uhamisho hadi saa moja usiku saa za Afrika mashariki , huku madirisha ya
uhamisho ya Uhispania, Ujerumani na Ufaransa pia yakifungwa siku ya leo.
BBC Michezo inaangazia baadhi ya wachezaji wa Ulaya ambao
huenda wakamia klabu mpya.
Ivan Rakitic
(Barcelona)
Kiungo huyu mwenye miaka 30 alikuwa anahusishwa na klabu ya Paris
St-Germain.
Kuwasili kwa Arturo Vidal na Arthur kunatoa ushindani mkubwa
kwa Ivan rakitric katika safu ya kati ya klabu ya Barcelona.
Huku hatma ya mchezaji wa Ufaransa Adrien Rabiot ikiwa
haijulikani katika klabu ya Paris St-Germain, klabu hiyo ya Ligue 1 inamnyatia
kiungo huyo wa kati wa Croatia na wanataka kuimarisha kitita cha uhamisho wake
cha Pauni milioni 112.
Jerome Boateng (Bayern
Munich)
Ni mlinzi mwenye umri wa miaka 29, ambaye pia anahusishwa na
klabu ya Paris St-Germain ya Ufaransa.
Uwezekano wa beki huyo wa Ujerumani Boateng kusalia na
mabingwa hao wa Bundesliga uko nusu nusu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City alihusishwa na
uhamisho wa Manchester United msimu huu, lakini klabi hiyo ya ligi ya dara la
kwanza huenda ndiko anakoelekea.
Shinji Kagawa
(Borussia Dortmund)
Ni kiungo Mjapani mwenye umri wa miaka 29 ambaye anahusishwa
na klabu za Sevilla ya Hispania na Olympique Marseille ya Ufaransa.
Kiungo wa kati wa zamani katika klabu ya Manchester United,
Kagawa hakushiriki katika mechi ya ufunguzi wa klabu ya Dortmund dhidi ya RB
Leipzig na ameripotiwa kutokuwa miongoni mwa mipango ya meneja mpya Lucien
Favre.
Huku mchezaji mpya aliyesajiliwa Axel Witsel na Thomas
Delaney wakitarajiwa, mchezaji huyo wa Japan alitarajiwa kuondoka katika Uwanja
wa Westfalenstadion katika siku ya mwisho ya uhamisho.
Claudio Marchisio (Huru)
Ni kiungo Mtaliano mwenye umri wa miaka 32 ambaye
anahusishwa na klabu za Porto na Benfica ya Ureno.
Kandarasi ya kiungo wa kati wa Italia, Marchisio katika
klabu ya Juventus ilikatizwa kutokana na makubaliano kati ya pande zote mbili
na sasa anatafuta klabu mpya.
Porto na Benfica wamehusishwa ijapokuwa klabu nchini Ureno
zina hadi tarehe 21 Septemba kufanikisha makubaliano yao.
Lazar Markovic
(Liverpool)
Kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 24 ambaye anahusishwa na
PAOK ya Ugiriki na Anderlecht ya Ubelgiji.
Ni kweli kwamba bado ni mchezaji wa Liverpool. Raia huyo wa
Serbia alijiunga na Liverpool kwa dau la Pauni milioni 20 kutoka benfica 2014,
lakini hajaichezea klabu hiyo tangu 2015.
Ruben Loftus-Cheek
(Chelsea)
Kiungo wa kati mwenye
umri wa miaka 22 ambaye anahusishwa na klabu ya Monaco ya Ufaransa na Schalke
04 ya Ujerumani.
Loftus-Cheek alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu
ya Crystal Palace, ambapo mchezo wake ulimfanya kuitwa katika kikosi cha timu ya
taifa ya Uingereza cha Kombe la Dunia kilichokuwa Urusi mwaka huu.
Huku Jorginho, N'Golo Kante, Ross Barkley na Mateo Kovacic
wakiwa mbele yake katika wachezaji wanaotarajiwa kucheza katika kikosi cha
kwanza cha timu katika klabu ya Stamford Bridge, Loftus-Cheek huenda akaanza kutafuta
klabu mpya.
Mario Hermoso
(Espanyol)
Beki huyo wa Espanyol ya Hispania mwenye umri wa miaka 23
anahusishwa na klabu ya Real Madrid.
Kuna kila uwezekano kwamba Real Madrid huenda ikaanza
kumtafuta kiungo wa kati anayetumia mguu wa kushoto iwapo Jesus Vallejo na
Hermoso watalengwa.
Hermoso alijiunga na Espanyol kwa dau la Pauni 360,000 msimu
uliopita na Real ina fursa ya kumnunua tena mchezaji huyo kwa dau la Pauni
milioni 13.5.
Comments
Post a Comment