- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA TIGANYA VINCENT, TABORA
VIGOGO wawili wa Benki ya Posta Tawi la Tabora na
mfanyabiashara mmoja waliokuwa
wanakabiliwa na jumla ya mashtaka saba ikiwemo utakatishaji wa zaidi ya
shilingi milioni 700 wametupwa jela miaka mitano au kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni mia moja
(100).
Mbali ya adhabu hiyo, Mahakama hiyo baada ya kuwatia
hatiani imewataka washtakiwa hao kulipa shilingi milioni 710
walizoiibia Benki ya Posta na vinginevyo mali zao zitaifishwe na serikali
kufidia kiasi cha fedha zilizoibwa.
Uamuzi wa shauri hilo la jinai Namba 154/2015 umetolewa jana
na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, Jocktan Rushwela, baada ya
kuwatia hatiani washtakiwa hao kwa makosa matatu kati ya saba.
Vigogo wa Benki ya Posta
Tabora waliopata adhabu hiyo ni Boaz Lunyungu aliyekuwa meneja, George
Ngatunga (Mhasibu) na mfanyabiashara Umaiya Makiliga.
Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa saa mbili Hakimu Rushwela aliwatia hatiani watuhumiwa
hao kwa makosa matatu kati ya saba waliyokuwa wanashitakiwa nayo ambayo ni kula
njma ya kutnda kosa la wizi, kutakatisha fedha na wizi.
Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili mwandamizi wa
Serikali Shedrack Kimaro aliiambia Mahakama hiyo kuwa watuhumiwa walitenda
makosa hayo kati ya Januari 2014 na Julai 2915 katika Benki ya Posta tawi la
Tabora.
Wakili Kimaro alidai
kwenye shitaka la kwanza kuwa katika kipindi hicho washitakiwa kwa
pamoja walikula njama ya kutenda kosa la wizi.
Ilidaiwa na wakili Kimaro kuwa washitakiwa wote watatu
katika tarehe tofauti kati ya mwezi Januari 2014 na mwezi Julai 2015 waliiba
jumla ya shilingi milioni 710 katika Benki ya Posta tawi la Tabora.
Shitaka la tatu ambalo lilikuwa likiwakabili aliyekuwa
meneja na Mhasibu wake ilidaiwa kuwa wakiwa ni watumishi wa Benki wa Posta
walitakatisha fedha shilingi milioni 710 huku wakijua wamezipata kwa njia
zisizo halali.
Upande wa jamuhuri wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo
ulileta jumla ya mashahidi 16 ambao waliweza kutoa ushahidi uliopeleka mahakama
kuthibitisha pasipo shaka kwamba watuhumiwa walitenda makosa hayo.
Mahakama imewahukumu kwenda jela miaka mitatu mitatu kwa
kosa la kula njama na lile la wizi na miaka mitano kwa kosa utakaktishaji wa
fedha, kwa vile adhabu hizo zinakwenda pamoja watutumikia kifungo cha miaka
mitano jela.
Washtakiwa hao watatu pamoja na kupata adhabu hiyo ya
kifungo bao wanakabiliwa na kesi nyingine ya kuhujumu uchumi wakiwa na watu
wengine 13 shauri amabalo bado alijaanza kusikilizwa kwani jalada lake lipo
ofisini kwa DPP likisubiri kutolewa uhamzi.
Comments
Post a Comment