- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imesaini mkataba wa kushirikiana na jimbo la Shandong na Hospitali ya magonjwa ya Moyo ya Fuwai iliyopo mjini Beijing nchini China.
Mkataba
huo ulisainiwa hivi karibuni nchini China na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi na Prof. Shengshou
Hu wa jimbo la Shandong mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya wa China Mhe. Xiaowei Ma.
Makubaliano yaliyosainiwa katika mkataba huo ni kutolewa kwa mafunzo
ya muda mrefu na mfupi kwa madaktari, wauguzi na wataalam wanaoendesha
mashine za moyo (Technician) na kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo
ambazo zitasaidia kuwajengea uwezo wataalam wa hapa nchini.
Katika
kutekeleza makubaliano hayo kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wataalam
watatu ambao ni Daktari, Muuguzi na mtaalam wa kuendesha mashine za moyo
(Technician) watakwenda katika Hospitali hiyo kwa ajili ya mafunzo ya
muda mfupi.
Hospitali ya Fuwai ni kituo cha kitaifa cha kutibu na chuo cha kufundisha wataalam wa magonjwa ya moyo ilianzishwa mwaka 1956 ina
wodi 41, vyumba vya upasuaji wa moyo 28, vyumba vya kufanya upasuaji wa
bila kufungua kifua kwa njia ya kutoboa tundu dogo katika mshipa mkubwa
wa paja au mkono (Cath lab) 13 na vitanda vya kulaza wagonjwa 1238.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
29/08/2018
Comments
Post a Comment