- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi wa Ajira Bw. Ally Ahmed
akizungumza na wajumbe walioshiriki kwenye kikao kazi cha kujadili mkakati wa
urasimishaji wa shughuli za sekta isiyo rasmi. (Kulia) ni Meneja wa Utafiti na
Sera kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Bi. Amina Ally Kutoka (SSRA). (Kushoto) ni Bi. Zahara Msangi kutoka Ofisi ya
Rais – TAMISEMI.
Meneja wa Utafiti na Sera kutoka Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Amina
Ally akifafanua jambo kwa washiriki walipokutana Jijini Dodoma.
Bi. Rehema Shao kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) akielezea jambo kwa wajumbe walioshiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada
walipokutana Agosti 28, 2018 Jijini Dodoma
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
…………………
NA MWANDISHI WETU
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na
Watu Wenye Ulemavu (Idara ya Ajira) kwa kushirikiana na taasisi na wadau
mbalimbali wameendelea na mkakati wa kupanga namna bora ya kurasimisha ajira za
sekta isiyo rasmi nchini.
Hatua hii ni katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama
Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 ambayo imeweka kipaumbele katika kuhakikisha
inaondoa umasikini kwa kuwawezesha watu walio katika sekta isiyo rasmi kuwa na
ajira au shughuli zenye tija kwa manufaa yao na manufaa ya nchi kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Mkurugenzi wa Ajira Bw.
Ally Ahmed alisema kuwa majadiliano haya yatachangia katika kuwatambua
wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara wadogo kwa kubaini mahitaji yao na
kuwawezesha kushiriki na kuchangia katika uchumi wa taifa letu.
“Urasimishaji huu utasaidia kutambua vikundi mbalimbali vya
wajasiriamali na wafanyabashara wadogo kwa kuzifanya shughuli zao kuwa zenye
manufaa makubwa na endelevu,” alisema Ahmed.
Aidha aliongeza pia, sehemu kubwa ya nguvu kazi ya taifa
letu ni vijana, hivyo urasimishaji wa shughuli zao kutawawezesha kutambulika,
kupata mitaji yenye masharti nafuu vilevile urahisi wa kuwapatia mafunzo ya
ujuzi na stadi za kazi katika kuboresha shughuli zao.
Kwa upande wake Bi. Rehema Shao kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) alieleza kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ilishaanza kusajili
wajasiriamali wa sekta isiyo rasmi kwa kuwapatia TIN na hivi karibuni tumeanza
kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara wadogo ili kuweza kuwatambua pamoja na
shughuli wazifanyazo.
“Ushirikiano wa wadau katika zoezi hili ni wa muhimu na ni
njia bora itakayopelekea matokeo chanya kwa kupunguza kiwango cha umasikini
pamoja na kuongeza walipa kodi kwa kuwawezesha wahusika kuwa na kazi za staha”
alisema Shao.
Mkutano huo umekutanisha wadau kutoka Ofisi ya Rais –
TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, MKURABITA, NSSF, TRA, TBS, TFDA, SSRA, CISO (T)
na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Comments
Post a Comment