- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu RITA Bw.
Charles Salyeem akitoa taarifa katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Waratibu Elimu
Kata na Maafisa Watendaji Kata kuhusu
Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa Shule za Msingi
na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga akifungua mafunzo kwa Waratibu
Elimu Kata na Maafisa Watendaji Kata
kuhusu Mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa
shule za msingi na Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28,
2018 mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga (kulia) na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah
wakiteta jambo wakati ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa
Watendaji Kata kuhusu Mpango wa Usajili
na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari
wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
PICHA DBaadhi ya viongozi wa Mkoa wa
Simiyu wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Maafisa
Watendaji Kata kuhusu Mpango wa Usajili
na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari
wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) unatarajia
kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi 60,000 wa shule za Msingi za
Sekondari wilayani Bariadi mkoani Simiyu, kupitia Mpango wa Usajili na kutoa
vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa miaka 06 hadi 18.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu RITA Bw.
Charles Salyeem wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na
Maafisa Watendaji Kata kuhusu Mpango wa
Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na
Sekondari wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 28, 2018 mjini Bariadi.
Salyeem amesema mpango huo utahusisha usajili na kutoa vyeti
vya kuzaliwa kwa wanafunzi wenye umri wa kuanzia miaka 06 hadi 18 kwa
ushirikiano kati ya RITA na Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia Idara
za Elimu ambapo wanafunzi watasajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa katika
shule zao.
Ameongeza kuwa watoto wa umri wa miaka 06 hadi 18 ambao si
wanafunzi watapata fursa ya kusajiliwa katika Ofisi za Watendaji wa Kata, huku
akibainisha kuwa watapaswa kuwa na viambatisho vya msingi vinavyotakiwa kwa
maelekezo watakayopewa na Watendaji wa Kata kwenye maeneo yao.
Aidha, Salyeem amesema wazazi na walezi wa watoto wenye umri
huo watahitajika kuchangia gharama kwa ajili ya usajili na kupata vyeti vya
kuzaliwa kwa watoto wao ili fedha
zitakazopatikana ziwezeshe kupeleka
mpango huu katika maeneo mengine.
Awali akifungua mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata kuhusu
mpango huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amewatakaWaratibu Elimu Kata na Maafisa
Watendaji Kata kuzingatia maelekezo watakayopewa na kufanya kazi kwa uadilifu
wakitanguliza uzalendo na siyo maslahi binafsi.
Aidha, Kiswaga amesema cheti cha kuzaliwa ni moja ya nyaraka
muhimu kwa wanafunzi wanaotoka hatua moja ya masomo kuingia nyingine hivyo
akawataka viongozi na watendaji kujipanga ili kuvuka lengo la RITA la kusajili
wanafunzi 60,000 kwa kuhakikisha kila fomu inayochukuliwa kwa ajili ya kuomba
usajili inarudishwa na cheti cha kuzaliwa kinachukuliwa.
“RITA imejiwekea lengo la kusajili wanafunzi 60,000 kati ya
zaidi ya 156,769 waliopo wilayani Bariadi, wanafunzi wasio na vyeti ni wengi,
hivyo basi tujipange tuweze kuvuka lengo, tutumie viongozi kuhamasisha wazazi
na kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa” alisema.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Ihusi, Kasimili Ngusa amesema
mpango huu utawarahisishia wanafunzi wengi wa umri wa miaka 06 hadi 18 kwa
kupata vyeti vya kuzaliwa shuleni walipo, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo
iliwalazimu wazazi na walezi kufuata huduma ya usajili na kupata vyeti vya
kuzaliwa Ofisi za Mkuu wa Wilaya.
Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Isanga, Sophia Kitobelo ametoa
wito kwa wazazi na walezi kutumia fursa hiyo ya kusajili na kuchukua vyeti vya
kuzaliwa shuleni na katika Ofisi za kata, kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata
vyeti vya kuzaliwa ambavyo ni miongoni mwa nyaraka muhimu kwa Watanzania.
Mkakati huu wa Usajili wa Wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari wenye umri wa miaka 06 hadi 18 umefunguliwa rasmi katika Wilaya ya
Bariadi na baadaye utaendelea katika wilaya nyingine za Mkoa wa Simiyu; hadi
sasa umeanza kutekelezwa katika wilaya kumi na moja za Mikoa miwili ya Dar es
Salaam, Mara na Njombe.
Comments
Post a Comment