- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA AFRIKA (AU) WAJADILI CHANGAMOTO ZA USAFIRISHAJI WA MIZIGO JIJINI DAR ES SALAAM
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) Usaje Asubisye katika semina ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika
(AU) waliokutana Dar es Salaam kujadili na kubadilishana uzoefu wa kutatua
changamoto hasa wanazokutana nazo katika usafirishaji mizigo kati ya nchi moja
na nyingine.
Baadhi ya viongozi katika semina hiyo
wakiwa wamekaa meza kuu wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Kamishna wa Forodha
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Usaje Asubisye hayupo pichani.
Picha mbalimbali zikionyesha washiriki
mbalimbali wanaoshiriki semina hiyo kutoka umoja wa nchi za Afrika AU semina
hiyo inafanyika kwenye jengo la ILO jijini Dar es salaam.
Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) Usaje Asubisye akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
washiriki mara baada ya kuizindua rasi leo.
NCHI wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wamekutana Dar es
Salaam kujadili na kubadilishana uzoefu wa kutatua changamoto hasa wanazokutana
nazo katika usafirishaji mizigo kati ya nchi moja na nyingine.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa
Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Usaje Asubisye wakati anafungua
semina kwa washiriki wa nchi hizo.
Amefafanua msingi wa kukutana kwao ni kujadili kwa kina
kutatua changamoto zilizopo na lengo lao ni kuhakikisha nchi za Afrika
zinashiriki kikamilifu katika kujenga uchumi.
Ametaja baadhi ya nchi ambazo zimeshiriki semina hiyo ni
Rwanda,Afrika Kusini, Kameruni, Every Coast na nchi nyingine za Afrika
Mashariki.
Amesema kuwa pamoja na mambo mengine watajadili namna ya
kuboresha utoaji huduma ya kusafirisha mizigo na kwa Tanzania nayo itatoa
uzoefu wake na namna ambavyo wamefanikiwa kuondoa changamoto.
“Afrika tunataka liwe bara ambalo litakuwa na uchumi imara
na hivyo kwetu sisi kupitia semina hiii tutaangalia nini kifanyike ili tupige
hatua,” ameongeza.
Ameeleza pia nchi za Afrika ambazo zinabandari kuweka
mkakati sahihi wa kusaidia nchi nyingine katika kusafirisha mizigo.
Pia amesema kuna baadhi ya changamoto ambazo zipo katika
nchi moja na nyingine hakuna kutokana na uwepo wa masuala ya sharia, hivyo
kupitia semina hiyo wataangalia namna ya kutua baadhi ya kero ili kurahisisha
usafirishaji bidhaa katika nchi hizo.
Kuhusu mafanikio Asubisye amesema awali kwa Tanzania
usafirishaji wa mizigo kutokea bandari ya Dar es Salaam hadi nchini Rwanda
zilikuwa zinatumika siku 12 lakini kwa sasa ni siku tano.
Akizungumzia zaidi changamoto ambazo wanaendelea kuzitafutia
ufumbuzi wake ni kwamba TRA inataka kuona idara na mamlaka za Serikali
zinafanya kazi kwa pamoja.
Amefafanua kwa sasa unaweza kukuta TRA wametoa kibali mzigo
usafiri lakini anapofika barabarani mzigo unazuliwa kwasababu ya kuzidi au
askari wa usalama barabarani nao wanakuwa na mambo yao na hivyo kusababisha
usumbufu.
Hivyo katika kushughulikia hilo wanataka wote ambao
wanahusika wanafanya kazi kwa pamoja kwani kuzuia mzigo kunasababisha
kuongezeka kwa gharama na athari zake zinamkuta mtumiaji wan chi nyingine.
Comments
Post a Comment