- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamuhuli
ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi akiteta jambo alipomtembelea
kumjulia hali Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya
Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono. Kushoto ni Mke wa Mzee Mwinyi,
Bi. Siti Mwinyi.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeketi (katikati) akiongoza
dua maalum kumuombea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla
(kulia)ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza
majeraha ya mkono. Aliyekaa kushoto ni Mke wa Mzee Mwinyi, Bi. Siti Mwinyi.
………………
RAIS Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi leo Agosti 29,2018 amemtembea na kumuombea dua
maalum Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya
Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti
4, mwaka huu Mkoani Manyara.
Mzee Mwinyi aliambatana na Mkewe Bi. Siti Mwinyi ambapo
wamemjulia hali pamoja na kufanya dua hiyo ili aweze kupona haraka kurejea
kwenye majukumu yake ya kitaifa.
“Nimefika leo kukujulia hali na upokee dua hii upone haraka.
Sisi tunaendelea kukuombea muda wote kwa muumba” alieleza Mzee Mwinyi.
Kwa upande wake Dkt. Hamis Kigwangalla amemshukuru Mzee
Mwinyi na Mama Mwinyi kufika kumjulia hali ambapo awali alimuelezea kuwa
anaendelea vizuri na muda wowote ataruhusiwa.
“Nashukuru kufika kwenu na sasa naendelea na mzoezi vizuri
huku kubwa nikisubiria ruhusa ya Madaktari wanaoendelea kunipatia matibabu”
alieleza Dkt. Kigwangalla.
Katika hatua nyingine kwa sasa Dkt. Kigwangalla afya yake
imeendelea kuimarika zaidi ambapo jana jioni ya Agosti 28, ameweza kutembea
umbali wa zaidi ya Kilometa Nane ambapo hii ni hatua nzuri kwani kila siku
amekuwa akiongeza umbali wa kutembea kwa lengo la kufanya mazoezi ya viungo
vyake.
Dkt Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya
Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa
kushoto.
Comments
Post a Comment