- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
MSAJILI NGOs AWAHIMIZA WADAU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUTILIA MKAZO UTEKELEZAJI WA SERA ZA MAENDELEO.
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Idara Kuu Maendeleo ya Jamii pamoja na
wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakisikiliza mada zilizokuwa
zikiwasilishwa kuhusu ushirikiano kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na
Serikali katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza
Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.

Na WAMJW Dodoma
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba
ameyataka wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutilia mkazo katika
kutekeleza Sera za Maendeleo zilizopo katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) ili kufanikisha
juhudi za Serikali katika kuletea wananchi Maendeleo.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha ushirikiano baina
ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini
ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.
Katemba amesisitiza kuwa Mashirika hayo yanapaswa
kuwasilisha mipango yao kwa Msajili ili kuweza kuwa na Mpango mkakati mmoja wa
kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
Ameongeza kuwa suala la Maendeleo ni mtambuka na linapaswa
kutekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, Wadau na wananchi ili kufanya
shughuli za Maendeleo kuwa endelevu.
Kwa upande wao wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
wakiwakilishwa na Mwakilishi wa Shirika la Care International Bi. Zenais Matemu
amesema kuwa wadau ni wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni muhimu katika
Maendeleo hivyo kuiomba Serikali kuendelea kushirikiana ili kufanikisha
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imepanga kukutana na wadau wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali mara moja kila baada ya miezi mitatu kujadiliana masuala
mbalimbali ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini.
Comments
Post a Comment