- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
MKUU WA WILAYA YA NEWALA AFANYA ZIARA KATIKA MIRADI YA KILIMO BIASHARA INAYOFADHILIWA NA SHIRIKA LA AGAKHAN FOUNDATION
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo
(mwenye pama), akishiriki utoaji chanjo ya ugonjwa wa kideri kwa kuku
alipozindua uchanjaji huo katika kijiji cha Chihangu Wilayni Newala.
NEWALA, MTWARA
Mkuu wa Wilaya ya Newala mkoani Mtwara Aziza Mangosongo amelipongeza
shirika la Agakhan Foundation kwa
kuwajengea uwezo wakulima katika Wilaya
hiyo.
Pamoja na pongezi hizo Mkuu huyo wa Wilya amesema Programu
zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua hali ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja,
vikundi na jamii ya wananchi wa Newala kwa jumla.
Mkuu huyo wa wilaya alisema hayo mapema wiki hii, akiwa
katika ziara ya mafunzo, Agosti 27, 2018, ambapo aliongozana na timu ya Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Newala
ili kujionea miradi ya vikundi vya
wananchi katika Halmashauri hivyo.
Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa wilaya aliongozana na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Rashidi Ndembo , Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya Mussa Chimae, Madiwani wawili wa Halmashauri ya Wilaya
pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya.
Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na ujumbe wake walitembelea
Shirika lisilo la Kiserikali la Aghakani Foundation (ARF) linaloendesha Program
ya Ajira na Ujuzi (Employment and
Skills) inayolenga kuwawezesha Kaya zipatazo 5000 za wakulima wadogowadogo kujiongezea kipato, kujipatia chakula na
kuongeza uzalishaji mali na kuongeza thamani ya mazao yao kwa Mikoa ya Lindi na
Mtwara.
Programu hiyo inayo miradi ijulikanayo kama Kilimo ni
Biashara unaotekelezwa katika Wilaya ya
Newala kuanzia April 2016 hadi Machi 2018, chini ya ufadhili wa shirika la Kijerumani lisilo la Kiserikali
la GTZ.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Newala alitembelea Vijiji vya
Chihanga, Idamnole, Tengulengu na Kitangari, mbapo akiwa katika Kijiji cha Chihangu yeye na msafara wake walikutana na
vikundi vya wakulima wanaofadhiliwa na
Aghakhan Foundation katika miradi ya
kuongeza kipato kwa kufuga kuku wa kienyeji kisasa, akashiriki kuzindua chanjo ya ugojwa wa kideri wa kuku unaoelezwa na wataalamu kuwa
ndiyo ugonjwa hatari wa kuambukiza
unaorudisha nyuma usalishaji wa kuku katika Wilaya ya Newala.
Akiwa katika Kijiji
cha Idamnole Kata ya Chihangu
alikagua shughuli ya ukamuaji wa mafuta
ya Alizeti unaofanywa na wakulima
katika vikundi vilivyo chini ya mradi wa kilimo Biashara unaofadhiliwa
pia na Aghakan Foundation, ambko aliona ujenzi wa nyumba bora ya mkulima
unaotokana na uzalishaji na bei nzuri ya
mauzo ya zao la korosho katika Mkoa wa Mtwara, hususani Wilaya ya Newala.
Tangu Serikali ya awamu ya tano chini ya Eais Dk. Jonh Magufuli iingie madarakani bei ya zao la
korosho imepanda na kuimarika hivyo kuwezesha wananchi kadhaa wa Wilaya ya
Newala kujenga nyumba nzuri na za kisasa, Vijijini.
Baadae msafara ulielekea katika Kata ya Kitangari Kijiji cha
Kitangari Tarafa ya Kitangari ambapo ulifika
kwa Wafugaji wawili wa kuku wanaofadhiliwa na Agakhan Foundation,
wakulima hao wameweza kuongeza uzalishaji wa kuku kiasi cha kufuga hadi kuku
800 wa chotara ambao kwa wastani mmoja huuzwa Sh.20,000 hadi Sh. 25,000 baada
ya kuhudumiwa kwa miezi minne tu.
Agosti 28, 2018, Mkuu huyo wa Wilaya Newala alitembelea
miradi ya kilimo cha Mbogamboga katika bonde la Chiunjila katika Kijiji cha
Chihanga Kata ya Mkunya na kisha kwenda Kijiji cha Mapili ambako alikutana na
mkulima wa nyanya na mfugaji wa kuku wa kienyeji ambaye anafuga kisasa baada ya
kupata mafunzo kutoka shirika lisilo la
Kiserikali la Agakhan Foundation.
Mkuu wa Wilaya alihitimisha ziara yake katika Kijiji cha
Nanguruwe.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Aziza
Mangosongo akiwa na ujumbe aliokuwa nao katika ziara hiyo.
Comments
Post a Comment