- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata
maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack
Kamwelwe kuhusu barabara ya juu ya
TAZARA wakati alipokagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar
es salaam Agosti 29, 2018. Kulia ni Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua hatua za mwisho za ujenzi wa
barabara ya juu ya eneo la TAZARA wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wa barabara za juu katika eneo la Ubungo jijini Dar es salaam Agosti
29, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi, Isack Kamwelwe na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es slaam, Paul
Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemaujenzi wa barabara ya juu
katika eneo la Tazara umekamilika kwa asilimia 98 na itafunguliwa Oktoba mwaka
huu na Rais Dkt. John Magufuli.
Mradi wa barabara ya juu (Mfugale flyover) chini ya ufadhili
wa Serikali ya Japani, unalengo la kupunguza msongamano wa magari katika
makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere.
Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 29 ,2018) baada ya
kukagua ujenzi wa mradi huowa barabara ya juu katika eneo la Tazara jijini Dar
Es Salaam.
Waziri Mkuu amesema ameridhishwa kazi ya umaliziaji wa mradi
huo inayoendelea kwenye hilo.
“Mradi utapunguza muda wa usafiri katika barabara ya Nyerere
hususani kwa wananchi wanaotoka katikati
ya jiji kwenda uwanja wa ndege na wanaotoka Buguruni, Temeke.”
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi Mkoa
wa Dar Es Salaam watafute eneo kwa ajili ya
wafanyabiashara ndogondogo ili waweze kuondoka kandokando ya barabara
hizo za juu zinazojengwa.
Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kukagua ujenzi wa
barabara za juu (interchange) eneo la Ubungo, katika makutano ya barabara za
Morogoro, Mandela na Sam Nujoma, eneo la Ubungo jijini Dar Es Salaam.
Amesema ni vema wafanyabiashara hao wakaondolewa na
kutafutiwa eneo lingine ili kulinda usalama wao kutokana na kazi za ujenzi
zinazoendelea kwenye maeneo hayo. Pia amewataka viongozi hao wawaelekeze
wananchi maeneo watakapowahamishia wafanyabiashara hao ili waweze kwenda
kununua bidhaa.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema mradi huo nao unalengo la
kupunguza msongamano wa magari kwa kutenganisha njia za barabara za Morogoro,
Mandela na Sam Nujoma ili kuwa na ngazi mbili juu ya barabara za sasa.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ujenzi wa mradi wa barabara ya juu katika eneo
la Tanzara (Mfugale flyover) unagharimu sh. bilioni 100.52 na unajengwa na
kampuni ya Sumitomo Mitsui ya nchini
Japan.
Amesema mradi huo umezingatia jinsi ya kuwezesha muunganiko
wa mfumo wa usafiri jijini Dar Es Salaam na ule wa mabasi yaendayo haraka awamu
ya pili, tatu na ya nne. “Tumeacha eneo la mita 12 katikati ya barabara kwa
ajili ya ujenzi wa mradi huo.”
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 28, 2018.
Comments
Post a Comment