- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja,
Kibaha Ramadhani Lutambi kupitia Chama Cha Chadema akiwapungia mkono baadhi ya
wananchi na wanachama wa CCM katika ofisi za CCM mkoani Pwani baada ya kuacha
chama hicho na kukimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM) (picha na Mwamvua Mwinyi).
Aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja,
Kibaha Ramadhani Lutambi kupitia Chama Cha Chadema amekimbilia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) (picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani Ramadhani Maneno
akizungumza baada ya kuwapokea madiwani watano kutoka upinzani na viongozi na
wanachama wengine wa vyama hivyo wapatao sita. (picha na Mwamvua Mwinyi)
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MADIWANI watano wa vyama vya upinzani ikiwemo Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, CUF na ACT Mzalendo na viongozi wengine sita
wamevikimbia vyama hivyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani.
Madiwani hao ni pamoja na Ramadhan Lutambi aliyekuwa diwani
wa kata ya Mailmoja kupitia Chadema na Ramadhan Kombe aliyekuwa diwani kata Mbwawa kupitia ACT.
Wengine ni, Muharami Mkopi Cuf kata ya Ruaruke wilayani
Kibiti,Seif Lwambo kupitia Cuf kata ya Beta,Muharami Mketo Cuf Kata ya Lukanga
na Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga.
Aidha viongozi waliojiuzulu kwenye vyama hivyo ni Ayubu
Chapile ambae alikuwa katibu kata ya Mkuza (CUF) ,Karimu Kasimu katibu tawi
chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere (Chadema) ,Selemani Mwinyimkuu mwenyekiti tawi
(Cuf),David Mramba Act,Latifa Sangalala mwanachama Chadema Mkoani B na Jumanne
Urembo Diwani kivuli ACT kata ya Sofu.
Awali Ramadhani Lutambi alisema ,chama kinachofaa kuongoza
nchi daima ni CCM kwani vyama vingine havina uwezo,na havijali viongozi wa ngazi za chini .
Alifafanua ,ameamua kuondoka Chadema ili kutekeleza yale
yanayofanywa na Rais Dk. Magufuli kwa wananchi wanyonge.
Lutambi alikiri kuondoka Chadema kwa hiari yake, kwa akili
zake timamu na kudai anajivua vyeo vyote alivyonavyo kuanzia sasa.
Akiwapokea madiwani na viongozi wa vyama hivyo kwenye ofisi
za CCM Mkoa, mwenyekiti wa CCM mkoani Pwani, Ramadhani Maneno alisema ,kutokana
na utekelezaji mzuri wa ilani wameona hakuna sababu ya kubaki kwenye vyama
vyao.
Alisema kazi kubwa inayofanywa na chama kupitia Rais Dk
.John Magufuli ndio sababu kubwa ya madiwani na viongozi hao kukimbilia CCM.
“Baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha kuwa wabunge,madiwani
na viongozi wanaohamia CCM wananunuliwa ,suala hili halipo ,ni kwamba wanarudi
kutokana na utendaji kazi wa chama chetu,” alisema Maneno.
Maneno alieleza, viongozi hao hawanunuliwi wala kuhongwa
bali ni mapenzi yao .
“Kuhusu gharama za uchaguzi kuwa ni kubwa hilo ni suala la
Tume ya Taifa ya Uchaguzi na chama kisilaumiwe kwani kuhama kwao hakuhusiani na
kurubuniwa ,” alisema Maneno.
Comments
Post a Comment