- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Exaud Mamuya (katikati) akiwakatika vazi maalumu baada ya kuchaguliwa kwamara nyingine kushika nafasi hiyo
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini
DIWANI wa kata Marangu
Mashariki katika jimbo la Vunjo,Mh Exaud Mamuya amechaguliwa kushika nafasi ya Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi baada
ya kushinda kwa kura 45 zilizopigwa .
Katika kinyang’anyiro hicho ,Mh
Mamuya alikuwa akichuana na wagombea,Filbert Shayo kutoka chama cha
NCCR-Mageuzi na Chata Madata wa Chama cha Mapinduzi ambaye hata hivyo baadae
alienguliwa.
Akizungumza wakati wa Uchaguzi
huo, Afsa Uchaguzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Patrick Nyavanga alitoa
ufafanuzi wa namna mshindi anavypatikana katika uchaguzi huo ikiwemo mshindi
kupata kura za ndio zisizopungua asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa.
Alisema uchaguzi huo
unafanyika kwa mujibu wa kifungu namba 6 cha kanuni za kudumu za Halmashauri na
baraza la madiwani wa Halmashauri wa Wilaya ya Moshi likaridhia kufanyika kwa uchaguzi
wa Makamu mwenyekiti.
Uchaguzi
huo ulilazimika kufanyika kwa awamu mbili baada ya awamu ya kwanza kukosekana
mshindi baada ya wagombea wote kutofikisha zaidi ya nusu ya kura zote
zilizopigwa.
Katika
marejeo ya awamu ya piliya zoezi la upigaji kura jumla yakura 45 zilipigwa ambapo
Mh,Mamuya alipata kura 45 baada ya mgombea kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi
Mhe,Shayo kuamua kujitoa wakati wa uchaguzi wa marudio na Mhe.Chata kuenguliwa.
Msimamizi
wa uchaguzi ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi Peter
Malendecha alimtangaza Mhe.Exaud Willison Mamuya mgombea kwa tiketi ya CHADEMA
kuwa Makamu Mwenyekitiwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwakipindi cha mwaka wa
fedha 2018/2019.
Akizuzngumza
mara baada ya kumtangaza mshindi,Malendecha alisema uchaguzi huo ulikuwa huru
na wa haki na umeendeshwa kwa amani na utulivu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu
na miongozo ya uchaguzi.
Mbali
na uchaguzi huo baraza la madiwa wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi limeunda kamati
na kufanya uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbalimbali za kudumu za Halmashauri
ikiwemo kamati ya Elimu ,afya na maji, kamati ya maadili, kamati ya mipango miji
na kamati ya Uchumi, ujenzi na mazingira.
Mwisho
.
Comments
Post a Comment