- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
- MWANAMKE
MMOJA MTAWA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KILE KINACHODAIWA KUJIRUSHA TOKA
GHOROFA YA PILI YA HOSPITALI YA BUGANDO HADI CHINI WILAYANI NYAMAGANA.
KWAMBA TAREHE 27.08.2018 MAJIRA YA SAA
05:00HRS ALFAJIRI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO ILIYOPO WILAYA YA
NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE MMOJA MTAWA AITWAYE SUZANA
BATHLOMEO, MIAKA 48, MKURUGENZI WA MIPANGO NA FEDHA WA HOSPITAL YA RUFAA YA
BUGANDO, ALIJIRUSHA TOKA GHOROFA YA PILI YA HOSPTALI YA RUFAA YA BUGANDO NA
KUDONDOKA CHINI. MTAWA HUYO AMEFARIKI DUNIA ASUBUHI YA LEO YA TAREHE
28.08.2018, WAKATI AKEIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO, NA KUPELEKEA
KUUMIA MAENEO YA KIUNO NA MGONGO, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
CHANZO CHA TUKIO HILO BADO
TUNACHUNGUZWA, HATA HIVYO UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA KUWA KATIKA OFISI
ALIYOKUWA AKIIFANYIA KAZI MAREHEMU AMBAPO YEYE ALIKUWA KIONGOZI ZIPO
TUHUMA ZA UPOVU WA FEDHA ZAIDI YA MILIONI MIA TATU, AMBAZO ZILIPELEKEA BAADHI YA
WATUMISHI WENZAKE KUSIMAMISHWA KAZI ILI KUPISHA UCHUNGUZI NA WENGINE KUFUKUZWA
KAZI.
AIDHA POLISI BADO WAPO KATIKA UPELELEZI
KUHUSIANA NA TUKIO HILO, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA
BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA
NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI JONATHAN SHANA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA
MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI
WANAPOONA WAMEKWENDA KINYUME NA TARATIBU ZA KAZI KAMA VILE KUJITOA UHAI AU
KUJIJERUHI KWANI NI KOSA KISHERI. AIDHA SAMBAMBA NA HILO ANAWAOMBA WANANCHI
WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU
NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI;
MNAMO TAREHE 23.08.2018 MAJIRA YA SAA
16:00HRS JIONI KATIKA MTAA WA NYAMHONGOLO WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA
MWANZA, ASKARI WAWILI AMBAO NI 1.H.5461 PC ENOCK WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA
MWANZA NA ASKARI 2.H.4165 D/C ROBERT WA KIKOSI MAALUMU, WALIKAMATWA KWA KOSA LA
KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI AMBAZO NI MENO MAWILI YA TEMBO, KISHA JANA
TAREHE 27.08.2018, ASKARI HAO WALIFUKUZWA KAZI, KITENDO AMBACHO NI KOSA
KISHERIA.
AWALI ZILIPATIKANA TAARIFA KUWA WAPO
WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA MENO YA TEMBO, NDIPO TAARIFA HIZO
TULIZIFANYIA KAZI KWA KUSHIRIKIANA NA KIKOSI CHA TAIFA CHA KUPAMBANA NA
UJANGILI KANDA YA ZIWA NA BAADAE TULIFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU
HUKU WAKIWA NA MENO HAYO MAWILI YA TEMBO. ASKARI HAO TUNATARAJIA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI SIKU YA IJUMAA YA TAREHE 31.08.2018.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI JONATHAN SHANA ANATOA WITO KUWA SHERIA NI MSUMENO,
SHERIA NI KWA WATU WOTE, SHERIA HAINA DINI, HAINA KABILA, SHERIA HAINGALII KAZI
AU CHEO CHA MTU, YEYOTE AMBAE NI MHALIFU MKONO WA SHERIA LAZIMA UCHUKUE HATUA
DHIDI YAKE. HIVYO TUTAWASAKA WALE WOTE MASWAHIBA WAO AMBAO WALIKUWA WANANUNUA
NA KUUZA MENO HAYO.
Comments
Post a Comment