- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MAHAKAMA ya Kisutu mjini Dar es Salaam imempata na hatia
mshindi wa Malkia wa Urembo nchini humo mwaka 2006 Wema Sepetu na kumpiga faini
ya shilingi milioni mbili za Kitanzania kufuatia kesi ya umiliki wa mihadarati
iliokuwa ikimkabili.
Aidha, mahakama hiyo imesema kuwa Wema atahudumia kifungo
cha mwaka mmoja iwapo atashindwa kulipa faini hiyo.
Wema Sepetu ambaye alishinda taji la malkia wa urembo nchini
humo 2006 atahukumiwa pamoja na washtakiwa wengine wawili Angelina Msigwa na
Matrida Seleman Abbas.
Hakimu Mkazi, Thomas Simba, aliambia mahakama hiyo siku ya
Jumatatu kwamba hukumu hiyo iliotarajiwa kutolewa siku ya Jumatatu sasa
itatolewa Ijumaa baada ya kukamilika kwa maswala machache yaliokuwa yamesalia.
Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 4 mwezi Februari mwaka
uliopoita, Wema na wenzake walipatikana wakimiliki misokoto ya bangi katika
eneo la Kunduchi Ununio.
Wema pia ameshtakiwa kwa kuvuta bangi.
Mwaka uliopita, maafisa wa polisi nchini Tanzania
walianzisha msako dhidi ya watu maarufu baada ya baadhi yao kuhusishwa na
ulanguzi wa mihadarati.
Mapema, mwanasheria mkuu Costantine Kakula, alisema kuwa
kesi hiyo iliwasilishwa mbele ili hukumu hiyo itolewe na kwamba upande wa
mashtaka ulikuwa tayari kusikiliza hukumu hiyo.
Kesi hiyo ilifikia awamu ya kutolewa kwa hukumu hiyo baada
ya mawakili wa walalamishi, Albert Msando na mwenzake wa upande wa mashtaka
Constantine Kukula kuwasilisha hoja zao za kwa nini washtakiwa hao wanapaswa
kupatikana na hatia au la.
Ilidaiwa kwamba mnamo tarehe 6 mwezi Februari, vitu hivyo
vilivyopatikana kutoka kwa washukiwa hao vilipelekwa kwa mwanakemia mkuu wa
serikali kwa uchunguzi na kuthibitishwa kwamba ushahidi huo ulikuwa gramu 1.08
za bangi.
Washukiwa 13 mahakamani kwa tuhuma za mihadarati Tanzania
Tarehe 8 Februari, washukiwa walipelekwa tena kwa mwanakemia
wa serikali ili kufanyiwa vipimo vya mkojo ambapo baada ya kuchunguzwa
ilibainika kwamba ilikuwa na bangi.
Hatahivyo upande wa malalamishi ulipinga matokeo hayo
ukisema kuwa yeye hupokea wageni wengi nyumbani kutokana na umaarufu wake.
Comments
Post a Comment