- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Dunia inapiga vita silaha za nyuklia na silaha za maangamizi (za kisayansi), lakini bado mataifa makubwa yanaendelea kutengeneza silaha nyingine nzito.
Silaha kama bunduki hazizungumzwi kabisa ingawa dunia inazungumzia amani. Kila siku wanasanyansi na wahandisi wanabuni silaha mpya. Je, hizi zinapelekwa wapi? Zinajaribiwa kwa nani kama si katika mataifa yanayoendelea hususan ya Afrika ambako mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ni kitu cha kawaida.
Anyway, lakini yote kwa yote ni kwamba, risasi zinazalishwa kwa wingi kama bunduki nazo zinavyozalishwa, na kwa kuangalia video hii, utashangaa ukiambiwa kwamba jumla ya risasi 1,000 zinatengenezwa ndani ya dakika moja.
Hii maana yake ni kwamba, kwa saa moja zinazalishwa risasi 60,000 na kwa kiwanda kinachofanya kazi kwa saa 12 maana yake jumla ya risasi 720,000 zinazalishwa - hii inamaanisha pia kwamba, kwa siku nzima (saa 24) jumla ya risasi 1,440,000 zinazalishwa.
Mungu tuokoe na hili balaa!!!
Comments
Post a Comment