- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS wa Tanzania John Pombe Magufuli ameibuka mshindi wa
Tuzo ya Afrika katika Masuala ya Uchumi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Ukombozi Afrika,
Mwebesa Rwebugia, ameieleza BBC kwamba Rais Magufuli ameibuka mshindi kutokana
na mchango wake wa kiuchumi hasa katika ukuaji wa miundo mbinu.
Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa Tanzania kupata tuzo
hii, baada ya Mwalimu Julius Nyerere kutuzwa pia kutokana na mchango wake wa
kuleta uhuru katika nchi za Afrika.
Mwebesa Rwebugia ameeleza kuwa, katika kuegemea kwenye
muktadha wa uchumi, kamati iliangalia umaskini ambao unatajwa kuwa adui mkubwa
anayefahamika, lakini pia maradhi na ujinga.
Kwa mujibu wa kamati hiyo ya Tuzo ya Ukombozi wa Afrika,
ukombozi katika kipengele cha elimu huangazia elimu na ujinga kama sehemu ya
ukombozi.
Tanzania imetolewa mfano wa elimu ya bila malipo kutoka
kutoka shule za msingi mpaka sekondari.
Katika suala la umaskini, kamati imeangalizia hatua ya
kuwajali watu wa kipato cha chini, ukitolewa mfano wa kusajiliwa kwa 'machinga'
katika kuwatambua rasmi kwa shughuli zao, na pia kuondolewa kodi za mazao kwa
wananchi.
Lakini siyo kila mtu amepokea vyema ushindi huu wa Rais
Magufuli kutokana na kwamba kiongozi huyo hajakamilisha hata miaka mitano tangu
aingie madarakani.
Wakosoaji wanasema amepunguza nafasi ya raia kujieleze kwa
uhuru.
Na serikali yake imekosolewa kwa hatua za kuvizima vyombo
vya habari na kinachotajwa kama kuvikandamiza vyama vya upinzani.
"Rais magufuli hakutazamwa kwa muda aliyoingia
madarakani lakini tangu miaka 20 iliyopita. Tangu alipokuwa wizara ya ujenzi na
mawasiliano na nyingine tofauti, mpaka kufikia hadi ya kuwa rais wa taifa. Je
ni mambo gani aliyoyafanya?" amefafanua Rwebugia.
Mnamo 2016 Magufuli alishinda tuzo ya Forbes Africa kwa kuwa
mtu anayeheshimika zaidi - na aliteuliwa kwa kutambulika jitihada zake za "kushinikiza
uchumi wa Tanzania."
Viongozi wengine walioishinda Tuzo ya Ukombozi:
Tuzo ya Ukombozi Afrika inatambuliwa barani Afrika na kimataifa
lengo lake ni kutambua mchango wa viongozi wa Bara la Afrika, wapigania uhuru,
wapatanishi wa amani na washiriki wengine wa Ukombozi wa Afrika.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni mwishoni mwa mwaka jana
aliwahi kuteuliwa mshindi na kamati inayoratibu Tuzo hiyo ya Ukombozi Afrika.
Ushindi wake Museveni ulitangazwa baada ya kamati hiyo
kuketi mwezi Oktoba, 2017 na kujiridhisha kupitia vigezo vilivyowekwa kuwa
kiongozi huyo anakidhi vigezo vyote.
Alitambuliwa miongoni mwa mengine kwa mchango wake mkubwa wa
kipekee alioutoa katika kusimamia amani katika nchi zilizokumbwa na migogoro ya
ndani Somalia, Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo na Burundi.
Vigezo vinavyozingatiwa pia ili kuteuliwa mshindi ni pamoja
na mchango wa kiongozi katika ukombozi wa taifa kutoka tawala dhalimu miaka ya
nyuma.
Viongozi wengine waliowahi kuishinda tuzo hiyo ni pamoja na
Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Kenneth Kaunda wa Uganda ambao
walitunukiwa tuzo hiyo mwaka 2014.
Rais Magufuli sasa anatarajiwa kupokea medali na cheti
katika tarehe rasmi itakayotangazwa na kamati baada ya maridhiano kati ya mgeni
rasmi na watu wa itifaki.
Comments
Post a Comment